Na.Khadija Seif,Michuzi TV
MJADALA wa Kitaifa wa Nishati safi ya kupikia umefunguliwa rasmi leo November Mosi Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) n kwa siku 2 ikiwahusisha wadau,taasisi mbalimbali kwa lengo la kujadili matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
Akizungumza
jijini Dar es salaam leo Novemba mosi Katibu Mkuu wizara ya Nishati
Felchesmi Mramba amesema tukio la mjadala huo unafanyika mikoa
mbalimbali ikiwemo Tabora,Shinyanga, Iringa,Dodoma na Morogoro huku
takribani mamilioni ya watanzania wakifatilia kupitia televisheni na
mitandao ya kijamii.
Aidha,
Mramba ameeleza kuwa mjadala huo ni safari ya awali ya kuhama kwenye
nishati isiyo salama ya kupikia na kuelekea nishati safi ya kupikia .
"Tunatambua
madhara yanayopatikana kwa kutumia nishati ya kupikia isiyo salama na
inaleta madhara mbalimbali ikiwemo athari kiafya,kiuchumi,kijamii hivyo
wadau na taasisi zitajadili namna ya taifa litahamia kwenye nishati safi
ili kuepuka matatizo yanayopatikana kwani waathirika ni vielelezo tosha
kuwa changamoto bado zinaendelea na jamii bado haijapata uelewa wa
namna ya kukabili changamoto za nishati isiyosalama.
Hata hivyo mjadala huo umehusisha wadau,taasisi na viongozi mbalimbali kiserikali pamoja na viongozi wastaafu.
Pia
Mramba amefafanua kuwa kuwepo kwa mjadala huu wa siku 2 ni ishara ya
wazi kuwa lengo la kumtua mama kuni kichwani litapata Suluhisho.
Mtaalam
mwandamizi wa maswala ya Fedha katika shirika la umoja wa mataifa wa
mitaji ya Maendeleo (UNCDF) Immanuel Muro akichangia mjadala wa
kupatikana kwa Suluhisho la kitaifa la Nishati safi ya kupikia na
kueleza kuwa bado asilimia kubwa jamii haina elimu ya kuelewa madhara
yanayopatikana katika nishati isiyo salama ya kupikia na kuepelekea
matumizi ya mkaa na kuni kuendelea kwa baadhi ya jamii.
Hata
hivyo Muro amesema kuwa ukosefu wa maji safi katika mkoa wa Dar es
salaam inawezwa kusababishwa na kukatwa kwa miti na misitu kwani mikoa
ya Lindi,Mtwara, Morogoro ndio mikoa inayotiririsha Maji kufika mkoa wa
Dar es salaam .
"50%
ya wakazi wa Dar es salaam wanatumia mkaa kam nishati ya kupikia
ambapo miaka mitano ijayo changamoto za kiafya zitazidi pamoja na
changamoto ya kimazingira itakbiliwa na ukame."
Pia
ametoa rai kwa Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka na kuhakikisha
jamii inapata uelewa na kutambua madhara yanayosababishwa na matumizi ya
Nishati ya mkaa na kuni.
Kwa
upande wake waziri mstaafu na Mkurugenzi mkuu mstaafu wa shirika la
umoja wa mataifa wa Makazi duniani (UN_Habitat) Anna Tibaijuka amesema
yeye ni mmoja ya mashuhuda wa watumiaji wa nishati ya kupikia ya kuni na
kukiri kuwa ametembea porini kutafuta kuni.
"Tuzungumze
mkakati wa kitaifa wa kuondokana na kuweza kupikia Nishati safi kiwe
kikao cha mkakati. Mpangilio ni nzuri na wale walio kwenye TV wanaona
kwamba Serikali yetu ina mpango Kwa kutusaidia akina mama."
Aidha,Tibaijuka
ametoa rai kwa serikali kuweka mkakati wa sera ya kitaifa ya kuweka
bei isiyobadilika badilka,mpango huu using kuwa kama Agizo tu Bali liwe
na mpango, sera na mazingira wezeshi kwa watu kumudu gharama hizo.
Mtaalam mwandamizi wa maswala ya Fedha katika shirika la umoja wa mataifa wa mitaji ya Maendeleo (UNCDF) Immanuel Muro Akizungumza juu ya umuhimu wa Nishati Safi na namna Mkaa unavyochangia kuharibu Mazingira
Mkurugenzi wa Taifa Gesi, Hamisi Ramadhani akichnagia katika Mjadala wa Kitaifa waNishati Safi ya Kupikia .uliofungiliwa leo jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Nishati ,January Makamba akiongoza Mjadala wa Kitaifa juu ya Masuala ya Nishati Safi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...