Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
BARAZA la madiwani Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,limemchukulia hatua ya kinidhamu mkuu wa idara ya ujenzi Brighton Kishoa kwa kumkata mshahara wake asilimia 15 ndani ya miaka mitatu , kutokana na uzembe kwenye usimamizi wa ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi na kuisababishia hasara Halmashauri hiyo.
Hatua hiyo ni fundisho kwa wakuu wa idara na watendaji wengine endapo watazembea na kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha,Mussa Ndomba alieleza maazimio hayo katika kikao cha robo mwaka baada agenda iliyojadili makosa ya kinidhamu ya mtumishi huyo ambae amekutwa na makosa ya uzembe na kushindwa kusimamia mradi huo.
Alifafanua, kamati za uchunguzi zimefanya kazi yake na kujiridhisha kuwa mkuu huyo wa idara amefanya uzembe.
"Hakuna anaependa kuchukuliana hatua kama hizi ,Ila inafikia hatua unachoka kutoa maagizo na kuelekeza kila wakati, adhabu hii anastahili kutokana na makosa aliyopatikana nayo ikiwemo usimamizi mbovu kwenye ununuzi wa vifaa na kusababisha gharama kubwa ya manunuzi wa vifaa kwenye ujenzi huo"aliongezea Ndomba .
Ndomba alitoa wito kwa watumishi wote hadi ngazi ya mtaa kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu bila kupingana na miongozo iliyopo.
"Kwa kutofuata miongozo miradi ya Serikali na utoaji huduma haitoonekana wala kuleta tija:" Hivyo asitokee mtumishi yeyote kuturudisha nyuma ,sisi kama Baraza tutakuwa wakali,hatutovumilia,kuona Mtendaji anazorotesha huduma kwa Wananchi,kuanzia sasa tutakuwa wakali, tutachukua hatua kwa wale wote watakaoonyesha utovu wa nidhamu kwenye utendaji kazi wao"alisisitiza Ndomba.
Vilevile, madiwani akiwemo diwani wa Kongowe Hashim Shomari, Diwani wa kata ya Tangini Mfalme Kabuga na diwani wa Visiga Kambi Legeza walieleza, wamechoshwa na changamoto zinazoelekezwa hospital ya Mkoani .
Kufuatia malalamiko hayo ,Baraza hilo limetoa wiki moja kwa idara ya afya kushughulikia baadhi ya changamoto zinazolalamikiwa katika hospital ya Mkoani .
Walieleza , hospital hiyo imekuwa ikitolewa malalamiko mengi hivyo idara ijitathmini ,na kujitahidi kutatua changamoto zinazoelekezwa katika hospital hiyo na baadhi ya Zahanati .
"Ifikie hatua ya kuona umuhimu wa maagizo na maelekezo mnayopewa na madiwani kila tunapokutana ,nendeni mkajitathmini na kufanya Yale ambayo yatapunguza changamoto zinazotajwa Mara kwa Mara ,"
Tunatoa siku 7 mkatatue mliyoelekezwa"jumatatu kamati ya fedha inakutana iidhinishe hata kama milioni 100 ili utekelezaji uanze"
Nae diwani wa kata ya Pichandege Karim Mtambo ,alihoji sh.milioni 800 zilizoidhinishwa kuendeleza ujenzi wa baadhi ya maeneo katika hospital ya wilaya ya Lulanzi ambayo tayarii imeshaanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Mtambo alisema ,imepita muda mrefu ,fedha hizo zipo Lakini hakuna muendelezo wa ujenzi, swali ambalo lilimuibua mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mshamu Munde na kusema awali zikitoka milioni 500 ambazo zimeshafanyiwa kazi.
Munde alibainisha kwamba ,milioni 800 ni fedha nyingine ambazo zipo kwenye hatua ya Ununuzi na kuanzia wiki ijayo zitafanyiwa kazi kulingana na maelekezo ya fedha hizo kwenye Maeneo ambayo ujenzi unaendelea ili kukamilisha hospital hiyo.
Alisema ,kamati ilihofia kutoa fedha kutokana na tatizo la maji ,Lakini alikaa nao na kuwaambia maji Ni moja ya vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi hivyo haiwezekani ujenzi ukasimama kutokana na malipo ya maji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...