Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi -Zanzibar imeipongeza Benki ya NMB kwa kuleta masuluhisho maalum yalio rafiki kwaajili ya wakandarasi huku akiamini ndio njia rahisi ya kusaidia kuwakuza wakandarasi wazawa kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed alipokuwa anazindua rasmi warsha ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi wa Zanzibar ikiwa na lengo la kuwatambulishia suluhisho mpya kwaajili ya wakandarasi na kuwasihi wachangamkie fursa hizo.

Mbali na hilo, Waziri huyo aliwasihi pia wakandarasi kutumia fedha za mikopo wanaopata kutoka kwa mabenki kwaajili ya kazi waliokopea na sio kwa shuguli zingine kwa inaweza wapa ugumu katika kurejesha mkopo huo.

Akizungumza katika warsha hiyo, mwakilishi wa Benki ya NMB ambae ni Mkuu wa Idara ya Miamala wa Benki hiyo, Bi. Linda Teggisa alisema kuwa Benki ya NMB imesimama katika nafasi ya kuendelea kuongeza fursa ya upatikanaji wa huduma za kifedha ili kuendelea kuwawezesha wakandarasi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za dhamana za zabuni kwaajili ya miradi au manunuzi (unsecured bid bond) pamoja na dhamana za utekelezaji (performance guarantee) au dhamana za malipo ya awali (advance payment guarantee), zote ambazo hazihitaji dhamana.

Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkuu wa wilaya ya Mjini, Mhe. Komred Rashid Simai Msaraka alisema kuwa sekta ya ujenzi imekuwa ni sekta ya muhimu sana kwa Zanzibar kwa sasa kwani ni miongoni mwa Sekta ambazo zinaongeza ajira zilizo na zisizo rasmi kwa wananchi wa Zanzibar na kupongeza taasisi za fedha kuamua kuongeza nguvu kwa sekta hii sio tu kuwanyayua wakandarasi lakini linaenda kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa Zanzibar

Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar, Bi. Naima Shaame (Kushoto) akizungumza katika warsha maalum ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi iliyolenga kuzitambulisha suluhisho mpya za benki ya NMB kwa wakandarasi. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano a Uchukuzi, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, wapili kulia ni waziri wa Ardhi, Mhe. Rahma Kassim Ali, kulia ni naibu waziri wa Ardhi, Mhe. Juma Makungu Juma na wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Miamala ya Benki ya NMB, Bi. Linda Teggisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...