MMkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa na Viongozi wa Nyati Cement, Viongozi wa Wilaya ya Kigamboni wakipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria Uzinduzi wa Stendi ya Kigamboni leo Novemba 8, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa akizungumza mara baada ya kuzindua na kupokea stendi ya Kigamboni iliyojengwa na Kampuni ya Nyati Cement Kigamboni.
Mkurugenzi Mkuuu Mtendaji wa Nyati Cement akizungumza wakati wakitoa maelezo ya mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Kigamboni leo Novemba 8, 2022.
Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Rahim Kondo akizungumza wakati wa makabidhiano ya Stendi ya Kigamboni iliyojengwa na Nyati Cement.
Diwani na Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Stephano Waryoba akitoa shukrani kwa kwa Nyati na Serikali ya Wilaya ya Kigamboni kwa kujengwa kwa Stendi ya Kigamboni katika Kata anayoiongoza.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa akipata maelekezo wakati alipotembelea katika Miradi mbalimbali inayojengwa katika Stendi ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa akitembele miradi mbalimbali inayojengwa katika Stendi ya Kigamboni.

KAMPUNI inayozalisha Sementi ya Nyati Cement imekabidhi kituo cha Daladala cha Kigamboni kwa Mkuu wa wilaya hiyo jijini Dar es Salaam leo Novemba 8,2022.

Akizungumza wakati wa Kukabidhi kituo hicho, Mkurugenzi Mkuuu Mtendaji wa Nyati Cement, Biswajeet Mallik amesema kuwa Kituo hicho kimegharimu shilingi milioni 46 katika ujenzi wake.

Amesema kuwa dhamira ya Kampuni hiyo ni kuhakikisha wanammunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuwaletea karibu huduma Wananchi.

Mallik amesema mbali na kusaidia kutengeneza kituo hicho teyari wamesaidia katika Sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu. Katika Sekta ya Afya wamesaidia katika Kituo cha afya cha Kimbiji, Kwa Upande wa Elimu wamekarabati Madarasa katika Shule ya Golani na Shule ya Sekondari Kimbiji pia wamesaidia Sementi katika ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kigamboni.

Akizungumzia kuhusu Miundombinu ambayo wanatoa huduma amesema kuwa Nyati Cement pia inatumika katika Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya (SGR) Pamoja na ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) kwenye bonde la mto Rufiji.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa akizungumza baada ya kukabidhiwa kituo hicho amesema kuwa kituo hicho kiwe fursa kwa wakazi wa Kigamboni kwaajili ya kujiletea Maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

"Sasa Nyati Cement wametusaidia hapa, tunakaribisha na tunawaomba wadau wengine, tutaendelea kuwapitia na kuwatafuta waendelee kushirikiana nasi ili waweze kuendeleza miradi hii kwa Manufaa ya Wananchi wetu na kwa Manufaa ya Wanakigamboni.

Stendi yetu tumeipokea tunashukuru na tutaendelea kuiangalia kwa jicho la kipekee, kwa Manispaa hili jambo lipo mikononi mwenu manispaa kuiangalia na kuhakikisha kwamba inafanya kazi Vizuri, wekeni Utaratibu mzuri na uangalizi mzuri lakini kuwapa utaratibu mzuri kwa Maendeleo ya wanakigamboni." Amesema Fatma

Amesema serikali ya wilaya ya Kigamboni ipo teyari kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha wanapata mabadiliko chanya ya haraka na yanayoleta maendeleo yenye tija kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Kigamboni

Pia ametoa Maelekezo kwa Manispaa ya Kigamboni washikamane na wale wanaowashika mkono nao kwa kutumia mapato ya ndani wahakikishe wanaboresha eneo la stendi hiyo ili kufikia malengo ya kuwa na stendi kubwa Kigamboni.

Amesema anaamini itakuwa stendi ya kipekee kwa Kigamboni na washirikiane mpaka eneo hilo la stendi lianze kufanya kazi kwa Ufanisi.

Kwa Upande wa Daladala Mkuu wa Wilaya amewaasa viongozi wasimamie Daladala ziweze kuanzia katika stendi hiyo kwa wale waliopewa kibali cha kuanzia katika stendi hiyo.

"Tutaweka Utaratibu Mzuri kama tulivyoshauriwa ili kuwabana wale ambao hawatakuja hapa, kwa Sababu eneo linalotumika kwa sasa sio eneo rasmi kwaajili ya stendi, eneo lile tunataka tuwaachie wenye eneo lao ili na wao waendelee na uwekezaji mwingine." Amesema

Kwa Upande wa Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Rahim Kondo amesema kuwa wameshaanza kutengeneza kibali cha Kuanzia katika stendi hiyo ambayo imekabidhiwa.

"Tunaamini kwa kuwepo hii Miundombinu itawezesha Magari kufanya kazi vizuri hivyo lazima washirikiane kupanga utaratibu mzuri." Amesema Kombo

Pia amewaomba Wamiliki na madereva wa magari wachukulie Chanya mabadiliko yatakayowekwa ili kuweza kuifanya stendi hiyo kukidhi vigezo vyake kama ambavyo vimekusudiwa pia amewaomba Halmashauri waendelee kuiboresha stendi hiyo kwa kuiweka iwe rafiki kwa watumiaji.

Kwa Upande wa Diwani na Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Stephano Waryoba amewashukuru Nyati Cement kwa kutengeneza stendi kwenye Kata yake kwaajili ya kurahisisha usafiri kwa wakazi wa kata hiyo na watumiaji wa stendi hiyo kwa ujumla. "Wananchi hizi sasa ndio fursa kwaajili ya maendeleo yetu sote."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...