Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WIZARA ya Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu imesema kwamba Serikali iliamua kusitisha kutoa vibali vya Watanzania kwenda kufanya kazi nchi kwasababu ya kutaka kuweka mazingira mazuri ya Watanzania kufanya kazi zenye staha na maslahi makubwa.

Imesema baada ya Serikali kujiridhisha na hatua ambazo imechukua katika jambo hilo ndio maana Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuruhusu kutolewa vibali kwa Watanzania wanapata ajira nje ya Tanzania kupitia Kampuni za Uwakala wa Ajira nchini.

Hayo yameelezwa leo Novemba 8,222 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri MKuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Profesa Jamali Adamu Katundu alipokuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kuwaaga Watanzania 50 kati ya 408 ambao wamepata kazi kwenye Kampuni ya Almarai ya nchini Saudi Arabia.

Watanzania hao wamepata ajira hiyo kupitia Kampuni ya Uwakala wa Ajira nchini Tanzania ya Bravo Job Agency inayomilikiwa na Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Temeke mkoani Dar es Salaam.

*Serikali iliamua kusitisha kutoa vibali vya ajira nchi ya nchi kwa lengo la kuweka mazingira mazuri na isitisha mwaka tangu mwala 2017,na baadae Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuruhusu baada ya kujiridhisha na Mazingira ambayo yamewekwa.Zamani Watanzania walikuwa wanapata kazi nje ya nchi lakini hizo kazi zilikuwa hazizingatii staha zao, maslahi madogo na namna ya uendaji wao ulikuwa hauna usimamizi na baraka za serikali, hivyo kukosa uangalizi,” amefafanua.

Ameongeza kuwa Rais ameruhusu baada ya kuona sasa hivi Mtanzania anapokwenda kufanya kazi nje ya nchi maslahi yake yamelindwa na Serikali inakuwa aliko na kazi anayokwenda kuifanya tofauti na zamani watu walikuwa wanakwenda bila utaratibu unaoeleweka.

Aidha, Profesa Katundu amesema serikali inatarajia kuona waliofanikiwa katika fursa hiyo na Watanzania wengine wanaopata nafasi ya kufanya kazi, wanafanya kwa uaminifu na uadilifu wakilinda heshima na hadhi ya nchi yao.

Amewataka Watanzania hao kuheshimu utaratibu na maadili ya nchi hiyo na kampuni watakazo fanya kazi ili kuimarisha uhusiano na kufungua milango ya wengine kuaminiwa na kuipa nchi sifa.

Pia, amesisitiza haja ya kufanya kazi kwa ushirikiano, kusaidiana na kuweka tofauti zao pembeni, huku wakitambua wameenda kufanya kazi na kwamba familia walizotoka na taifa linawategemea katika kuinua uchumi huku akitoa pongezi kwa Kampuni ya Bravo Job Agency kwa kushiriki kusaidia kutatua changamoto ya ajira nchini kwa kuangalia fursa kwenye nchi nyingine.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA), Joseph Nganga alisema hatua ya Watanzania hao imezingatia utaratibu wa ajira na serikali imehakikisha maslahi yao yanakidhi kazi wanazoenda kufanya.“Siwezi kutaja viwango vya mishahara lakini hakuna ambaye atalipwa chini ya sh. milioni moja, tumehakikisha hata saa za ziada za kazi zinalipwa na stahiki muhimu ikiwemo bima, malazi na usafiri watahudumiwa."

Ameongeza kwamba ajira hizo ni hatua ya serikali kupunguza wimbi la mahitaji yaliyopo na kuinua uchumi huku akifafanua kwa kutoa mfano kwamba kama Watanzania hao wakiamua kuleta sehemu ya fedha zao nchini zinaweza kufanya maendeleo makubwa.

Akizungumza kwa njia ya mtandao Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini, amewataka vijana hao 50 kuhakikisha wanapofika nchini humo wanafuata tamaduni za nchi hiyo, huku akiwataka wawe waaminifu muda wote watakaokuwa wakifanyakazi.

Amesisitiza haja ya kuwa karibu na ubalozi na wasigeuze ofisi hizo kituo cha polisi, ambapo kufika siyo lazima wawe na kesi au matatizo.

Mmoja wa Watanzania wanaosafiri kwenda kuanza kazi nchini humo Haji Bakari, ameihakikishia serikali watakuwa mabalozi wa kuitangaza Tanzania kwa kufanya kazi kwa uadilifu, umoja na mshikamano ikiwemo kuzingatia utamaduni za taifa hilo.

Kwa upande wake, Mtemvu amesema uamuzi wa serikali chini ya ya Rais Samia kutoa kibali kwa Watanzania kuendelea kufanya kazi nje ya nchi tangu mwaka 2017 vilipofungwa, ni ya kipekee.
"Nashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi huu wa kuruhusu Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

"Huko nyuma ilizuiliwa na nakumbuka wakati wanazuia Nilikuwa na vijana ambao walishakuwa na tiketi zao mkononi, nilipitia wakati mgumu lakini nashukuru niko salama.Kila wiki vijana 50 watakuwa wanaondoka kwenye Saudi Arabia kwa ajili kwenda kufanya kazi."


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Profesa Jamal Adam Katundu(wa pili kushoto) akiwa ameshikana mkono na Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Ajira nchini Tanzania Bravo Job Agency Abbas Mtemvu(wa pili kulia) bada ya Serikali kumbidhi vibali vya watanzania 50 ambao wamepata ajira nchini Saudi Arabia katika Kampuni ya Almarai.Watanzania hao wanatarajia kuondoka nchini kesho na leo wameagwa rasmi. Wakwanza kushoto ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania Bwana Fahad na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Hemed Mgaza.

Mwakilishi wa Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania Bwana Fahad akitoa salamu za kuwakarabisha watanzania 50 wanaokwenda kwenye nchi hiyo kwa ajili ya kufanya kazi katika kampuni ya Almarai baada ya kupata ajira.(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE-MICHUZI TV)

Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Ajira nchini Tanzania Bravo Job Agency Abbas Mtemvu akipitia baadhi ya nyaraka kabla ya kuzungumza na watanzania wanaotarajia kwenda nchini Saudi Arabia baada ya kupata ajira kwenye Kampuni ya Almarai.

Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Hemed Mgaza(kulia) akiteta jambo la Mwakilishi wa Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania Bwana Fahad (kushoto).

Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Ajira nchini Tanzania Bravo Job Agency Abbas Mtemvu akifafanua jambo wakati wa kuagwa kwa watanzania 50 wanaokwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia.Mtemvu ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali anayoingoza kwa kuamua kuruhusu kutolewa vibali Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Hemed Mgaza akizungumza wakati wa tukio la kuwaaga Watanzania 50 wanaokwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia baada ya kupata ajira katika Kampuni ya Almarai iliyoko kwenye nchi hiyo.


Sehemu ya wafanyakazi wa TaESA(waliovaa shati rangi nyeupe) wakiwa kwenye tukio la kuagwa kwa watanzania 50 wanaokwenda nchini Saudi Arabia kufanya kazi.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) Joseph Nganga akielezea hatua kwa hatu namna ambavyo wamehakikisha tararibu zote zimefuatwa kwa Watanzania hao kabla ya kuondoka kwenye nchini Saudi Arabia kufanya kazi kwenye kampuni ya Almarai.

Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Profesa Jamal Adam Katundu(kulia) na Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Hemed Mgaza(kushoto) wakijadiliana jambo wakati wa tukio la kuaga watanzania 50 wanaokwenda nchini Saudi Arabia kufanya kazi kwenye kampuni ya Almarai.

Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Profesa Jamal Adam Katundu akizungumza na waandishi wa habari wa kuagwa kwa watanzania 50 ambao wanakwenda nchini Saudi Arabia kufanya kazi baada ya kutafutiwa ajira kwenye kampuni ya Almarai kupitia Kampuni ya Uwakala wa Ajira nchini Tanzania Bravo Job Agency.



Baadhi ya vijana wa kitanzani ambao wamepata ajira katika Kampuni ya Almarai ya nchini Saudia Arabia wakiwa makini kufuatilia maelezo kutoka kwa viongozi mbalimbali walipokuwa wakiagwa leo Novemba 8,2022 kwa ajili ya kuelekea Saudia Arabia kesho Novemba 9,2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...