Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Timu ya taifa ya Uingereza imepata ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya timu ya taifa ya Iran kwenye mchezo wa Kundi B uliopigwa kwenye dimba la Kimataifa la Khalifa mjini Doha katika Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.

Kwenye mchezo huo Nyota wa timu ya taifa ya Uingereza wameendelea kung’ara kama wapo kwenye Ligi yao ya nyumbani ya ‘English Premier League’ (EPL)!

Mabao ya Uingereza katika mchezo huo, yamefungwa na Jude Bellingham dakika ya 35', Bukayo Saka dakika ya 43' na 62', mabao mengine yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 45+1', Marcos Rashford dakika ya 71', Jack Grealish dakika ya 90.

Mabao mawili ya timu ya taifa ya Iran, yote yamefungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo, Mehdi Taremi dakika ya 65' na 90+13' kwa mkwaju wa Penalti.

Kundi B la Michuano hiyo lina timu za Uingereza, Iran, Marekani na Wales.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...