Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire na mkuu wa shule ya sekondari Dodoma, Francis Tumaini wakifungua pazia ili kuzindua darasa la Tehama ambalo limewekewa vifaa na kampuni hiyo, vifaa hivyo ni Kompyuta 15, Meza 15, viti 15, Televisheni moja, kifushi cha intaneti kwa mwaka mmoja ambapo msaada huu umegawiwa ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kidijitali lakini pia kuwawezesha wanafunzi kusoma somo la Kompyuta ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire akikata utepe kwenye moja ya madawati yaliyo na vifaa vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa shule ya sekondari Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire akimuuliza swali dada mkuu wa shule ya sekondari Dodoma kuhusu namna ‘Coding’ inavyomsaidia katika kujifunza darasani, binti huyo ni mojawapo ya wasichana wanaosoma tahasusi (Combination) mpya ya Fizikia, Hisabati na Sayansi ya Kompyuta (PMC) ambapo msaada uliotolewa na kampuni hiyo utawasaidia katika kujifunza zaidi. Wanaoshuhudia ni wanafunzi wa kike wanaosoma tahasusi hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na waalimu wa shule ya sekondari Dodoma mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya Tehama shuleni hapo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...