*Ni kutokana na kuchangia Mto Ruaha kukauka na kuleta madhara
*Mwakilema :Ihefu ambayo ni tegemeo yaingiliwa na kilimo na ufugaji

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv, Msembe ,Iringa
SERIKALI imesema kuwa waliopo katika vyanzo vya Maji wasitishe shughuli zao za kilimo kutokana na kuchangia kukauka kwa mto Ruaha Mkuu.

Hayo ameyasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dk.Seleman Jafo kwenye mkutano wa mawaziri nane uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Ruaha iliyopo Msembe mkoani Iringa.

Kabla ya mkutano huo umechukua masaa matatu ya viongozi kujadiliana kutokana na hali waliokuta katika mto Ruaha ukiwa umekauka.

Dk.Jafo amesema kukauka mto Ruaha umeathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo mgao wa umeme pamoja kutokuwa na maji ya matumizi ya nyumbani katika mkoa wa Dar es Salaam.

Dk.Jafo ameagiza bodi za bonde za maji na Baraza la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira kusimamia vyanzo vya maji kwa wale waliochepusha na wale wanaotumia maji kwa mujibu wa vibali kuangalia suala hilo.

Amesema kuwa suala la Ruaha tangu 1994 maji yanaacha kutiririka mwezi wa tano hiyo ni kutokana na shughuli za kibidamu kuendelea kwenye vyanzo vya maji.

Aidha amesema kwa kipindi hiki wanyama wakiwemo viboko wako katika hali mbaya hivyo tuombe mvua zinyeshe kwa kipindi kifupi viboko hao waendelee kuishi vinginevyo watakufa.

Naye Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema amesema ukame wa Mto Ruaha ni hatari kwa wanyama na hii ni kutokana bonde la Usangu/Ihefu kuendelea kwa shughuli za kilimo za kuzuia maji kwenye mto Ruaha.

Mwakilema amesema jitihada mbalimbali zinafanyika za kuweza Mto Ruaha kuwa na maji kwa vipindi vyote kutokana na mto huo kuwa na tegemeo kwa Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa  Rais Mazingira na Muungano  Dk.Seleman Jafo akizungumza na mawaziri na viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa kujadili kukauka kwa mto Ruaha Mkuu na madhara yaliyotokea kwenye Mto huo Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Ruaha Msembe ,Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi Chana akitoa maelezo kuhusiana na mto Ruaha Mkuu na madhara kwa wanyama kwenye Mkutano  wa Mawaziri Nane waliofika kujionea kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu uliofanyika Makao Makuu Hifadhi ya Ruaha Msembe,Iringa


Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika  la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema akionesha kukauka Mto Ruaha wakati Mawaziri Nane waliofika hapi kuangalia Mto huo Msembe Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...