Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kwa Mbegu iliyopo Kata ya Maore Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau kupitia kazi za sanaa ya uchoraji kuwatafutia soko la uhakika la bidhaa za picha zinazoonesha vivutio vya utalii, mila na tamaduni zetu.

Wamesema hayo wakati wakiwaonesha kazi za sanaa ya uchoraji wadau wa utalii kutoka Taasisi isyokuwa ya kiserikali ya KATIE ADAMSON CONSERVATION FUND ya nchini Marekani na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Women Youth Empowerment CONSERVATION ya nchini Tanzania walipotembelea shule hiyo.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao; wanafunzi Rajabu Ramadhani Mshana na Oda Ramadhani wamesema endapo watapatiwa soko la Uhakika itawasaidia kukuza kipato chao kwani kwa sasa picha moja wanauza kwa shilingi za Kitanzania elfu 45 Katika hifadhi ya Mkomazi.

Wamesema kupitia kazi ya sanaa ya uchoraji wa picha imewasaidia kupata kipato ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili pindi mzazi anaposhindwa kulipia gharama za shule.

Kwa upande wake mwakilishi wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Krisensia Masawe amesema kazi ya sanaa ya uchoraji wa picha imewasaidia wanafunzi hao kuongeza maarifa nje ya darasa na pia fedha zinazotokana na biashara ya picha zimesaidia kununua vifaa mbalimbali vya kufundishia shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea kupata kipato pindi atakapohitimu masomo yake na kujiajiri kupitia sanaa hiyo.

Mkurugenzi wa Taasisi isyokuwa ya kiserikali ya KATIE ADAMSON CONSERVATION FUND Bwana Dave Johnson ameahidi kuendelea kuwasaidia wanafunzi hao kwenda picha hizo nchini kwao, ili kuandika kitabu kupitia utalii uliopo nchini Tanzania, na kuhamasisha watalii kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii pamoja na shule hiyo.

Aidha Mwanzilishi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Women Youth Empowerment CONSERVATION ya nchini Tanzania ambaye pia ni muhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa Bwana Abel Mtui amesema lengo kubwa la mradi huo ni kuwajenga watoto kupenda uhifadhi na kutunza wanyamapori.

Amesema kupitia sanaa hiyo ya uchoraji wa picha imekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kuwauzia watalii wanapotembelea shuleni hapo na hifadhi ya mkoazi iliyopo jirani na shule hiyo kwa lengo la kukuza maarifa na kipato kwa ujumla.

Shule ya Sekondari Kwa Mbegu ina jumla ya wanafunzi 645 ambayo ni ya mchepuo wa Sayansi na Sanaa.

Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Taaisi ya katie Adamson Conservation fund DAVE Johnson iliyoko Marekan,Kushoto Abel Mtui Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa iliyopo Morogoro
 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...