Na Mwandishi Wetu
Wenyeji wa Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022, timu ya taifa ya Qatar wameaga mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kufungwa mabao 3-1 na timu ya taifa ya Senegal katika mchezo wa Kundi A uliopigwa dimba la Al Thumama mjini Doha.

‘The Maroon’ wakiwa kwenye ardhi ya nyumbani wakiongozwa na Kocha raia wa Hispania, Félix Sánchez Ba wamejikuta wakitupwa nje ya Michuano hiyo, baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo wakiwa Kundi A la Michuano hiyo mikubwa ulimwenguni.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Ecuador walipokea kichapo cha mabao 2-0 ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa Michuano hiyo, Novemba 20 mwaka huu, mabao yote mawili yalifungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo ya Ecuador, Enner Valencia.

Mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Simba wa Teranga (Teranga Lions), Senegal, timu ya taifa ya Qatar wamekutana na kichapo kingine cha mabao 3-1, mabao hayo ya Simba wa Teranga yamefungwa na Boulaye Dia dakika ya 41’, bao la pili lilifungwa na Famala Diedhou kwenye dakika ya 48’ na bao la tatu likifungwa na Bamba Dieng dakika ya 84’ huku bao la Qatar likifungwa na Muhammed Muntari.

Msimamo wa Kundi A, Uholanzi wanaongoza Kundi hilo wakiwa na alama zao 3 wakicheza mzunguko mmoja pekee, nafasi ya pili akiwa ni Educator wenye alama tatu wakiwa na mzunguko mmoja pekee, nafasi ya tatu ni Senegal wenye alama tatu, wakiwa na michezo ya mizunguko miwili na Qatar wanaburuza mkia bila alama yoyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...