Na John Walter-Manyara
Vijana mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kufanya ziara ya siku mbili mkoani hapa.
Wito huo ameutoa Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi wakati akizungumza na vijana wa Chama hicho mjini Babati ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 22 na 23 mkoani Manyara.
Kenani amesema amefika katika mkoa wa Manyara kwa ajili ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuungana na vijana na kuwahamasisha kupitia Kauli mbiu yao isemayo 'Alipo Mama, Vijana tupo".
Amesema vijana lazima wamtie moyo Rais na kumuheshimisha kupitia mapokezi yatakayofanyika.
"Lazima mapokezi ya Rais katika mkoa wa Manyara yawe ya kipekee tofauti na mikoa mingine ambayo ameshakwenda" alisema Kenani.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Manyara Inyasi Amsi amesema Ugeni ni wa kwao Manyara na ni vijana hawana budi kujitokeza kuhamasishana kumlaki Rais.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...