Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji
WATANZANIA wametakiwa kuenzi juhudi za muasisi wa Taifa letu Bibi Titi Mohammed ambae alishiriki kumkomboa Mwanamke na kumng'oa mkoloni kwa maslahi ya Taifa na vizazi vijavyo.

Akimuelezea hayat Bibi Titi wakati wa Kongamano la kumuenzi muasisi huyo lililoandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Rufiji kwa kushirikiana na ofisi ya Mbunge Mohammed Mchengerwa, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda alieleza , Mwanamke huyo alikuwa jasiri mwenye misimamo mikali kulipigania Taifa na kumkomboa mwanamke.

"Muasisi huyo atakumbukwa pamoja na baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere kwa harakati zao za kulikomboa Taifa"alisema Chatanda .

Aidha alieleza Bibi Titi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania na amezidi kukumbukwa na Jumuiya ya wanawake kwa kuenzi yale aliyokuwa akiyafanya kwa vitendo.

"Leo hii tunamshuhudia Rais Samia Suluhu Hassan akifuata nyayo za Bibi Titi kwa kupigania usawa wa Maamuzi na uongozi kwa wanawake pamoja na kupambana na vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake"alieleza Chatanda.

Awali mwanae Bibi Titi ,aliyejitambulisha kwa jina la Halima alisema , Bibi Titi ni mwanamke aliyejitoa mhanga kwa Ukombozi wa Watanzania.

Alisema ,pia alipenda haki kwa mwanamke ,na alipenda kuona mwanamke anashika nafasi mbalimbali za Uongozi hadi Urais .

"Cha ziada alikuwa nyakanga na mwana sanaa ,alikuwa na sauti nzuri, alikuwa na kipaji kutoka kwa kizazi chake ambapo aliimba wimbo wa Hongera Mwanangu na baadae wimbo huu kuwa maarufu baada ya Issa Matona kuuenzi na wimbo huo kuendelea kutamba hadi leo"alielezea Halima.

Mwanasiasa mkongwe nchini Kate Kamba alieleza anavyomfahamu Bibi Titi Mohammed katika siasa, mwanaharakati kuwang'oa wakoloni pamoja na kumkomboa mtoto wa kike kupata elimu sawa .

Alieleza Bibi Titi alikuwa mwanamke mwenye misimamo mikali ,na kutoa wanawake ndani kwenda kushiriki katika mikutano na siasa .

Kate alielezea ,muasisi huyo alikuwa shujaa ,mwenye maono makubwa kumkomboa mwanamke , mwanamke mwenye mipango na kupigania elimu kwa watoto wa kike na ndio maana alihakikisha wajukuu zake wanasoma.

"Tulimhangaikia mjukuu wake wa mwisho Dola kumpambania mjukuu wake huyo anasoma Canada ,na wajukuu zake wote walisoma ,aliwalea kwa kuhakikisha wanasoma"alisema Kate.

Alifafanua,Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi wafuate nyayo zake katika ujasiri wa kupita kuwavuta wanachama wapya, yeye aliweza kuwavuta wanachama zaidi ya 5,000 kujiunga na TANU na alifanikiwa.

Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo na ambaye pia ni mbaraza Mariam Ulega alisema ni jambo la faraja , Wanawake Mkoa wa Pwani kwa kufanya maadhimisho ya kumbukumbu hayo katika Mkoa huo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake ,Mkoa wa Pwani Zainabu Vulu aliwapongezi Wanawake kwa jinsi ambavyo wamejitokeza katika maadhimisho hayo.

Mwaka 1926 Bibi Titi alizaliwa ambapo Tarehe 5 Nobemba 2000 alifariki kwenye hospital ya Net Care Hospital Mjini Johannesburg ambako alikuwa akitibiwa.

Moja kati ya barabara kubwa ya Jijini Dar es Salaam limepewa jina la Bibi Titi Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.

Picha mbalimbali za Kongamano la kumuenzi muasisi Bibi Titi Mohammed lililoandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Rufiji kwa kushirikiana na ofisi ya Mbunge Mohammed Mchengerwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...