Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), leo Desemba 22, 2022 imekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima.

Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Mej. Jenerali (Mstaafu), Hamis Semfuko, umetumia nafasi hiyo kueleza dira na malengo ya TAWA katika tasnia ya uhifadhi na utalii.

Mazungumzo hayo yalijikita katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA ndani ya Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima akiwa kwenye picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Mej. Jenerali (Mstaafu), Hamis Semfuko.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Mej. Jenerali (Mstaafu), Hamis Semfuko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...