Na Pamela Mollel,Arusha

Chuo cha Uhasibu Arusha kimepongezwa kwa kuboresha mitaala ya utoaji wa mafunzo kwa vitendo ukilinganisha na vyuo vingine hapa nchini

Akizungumza katika mahafali ya 24 ya chuo hicho Mkaguzi wa ndani wa serikali Athuman Mbutuka kwa niaba ya waziri wa fedha na mipango dtk Mwigulu Nchemba

Alisema kuwa kutokana na chuo hicho kuwa na mitaala mizuri ya ufundishaji ni vema vyuo vingine vikaiga mfano huo.

Aidha ametoa wito kwa vyuo vyote hapa nchini kupitia na kuhuisha mitaala yao katika fani za biashara na uongozi ili kuhakikisha fani hizo zinajumuisha kikamilifu stadi za tehama.

Awali kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Dkt Cairo Mwaitete amesema kuwa chuo cha uhasibu Arusha wana mpango wa kuongeza wataalamu na walinzi wa kupambana na wadukuzi wa mitandao ambao kwa sasa unaikabili jamii.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa masomo 2021/2022 Chuo kimefanya jitihada za kuboresha miundombinu ambazo zinaendelea mpaka sasa

"Katika kipindi hicho chuo kimejenga majengo mawili moja ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 4000 kwa wakati mmoja na lingine likiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3000"alisema Mwaitete

Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha uhasibu Arusha la dkt Mwamini Tulli amesema kuwa wahitimu waliohitimu wana ongezeko la wahitimu elfu moja wa mwaka jana.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu waliohitimu chuoni hapo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala amesema kuwa moja ya mambo aliyojifunza ya kuweza kusaidia jamii.ni tehema kwani yanasaidia katika uongozi na utatuzi wa migogoro.

Katika chuo hicho jumla ya wahitimu elfu tatu 3529 wameweza kutunukiwa veti vyao katika ngazi nne tofauti za astashahada ,sstashahada ,shaada, na shaada za uzamili 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...