Na Mwamvua Mwinyi-Pwani


LASMIN KONDO mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Masaki , wilayani Kisarawe Mkoani Pwani,amekutwa akiwa amejinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa jeshi la polisi mkoani Pwani ,ACP -PIUS LUTUMO anasema ,ni matukio mawili ya watu wawili kupoteza maisha katika matukio mawili tofauti yaliyotokeza wilayani Kisarawe.

Akielezea tukio la kwanza, alieleza mwanafunzi huyo amejinyonga baada ya kugombezwa na wazazi wake kutojihusisha na matukio ya mapenzi kufuatia kukutwa na barua aliyokua amemuandikia mpenzi wake.

Katika hatua nyingine,kamanda LUTUMO ameeleza kuwa PILI MANG'OTA ambae ni mkulima wa mboga mboga na mkazi wa Sanze Kisarawe ,amekutwa amefariki dunia.

"Mwanamke huyu aliaga kwenda Visegese kuchukua mboga lakini hakurudi tena hadi umauti ulipomkuta na kukutwa vichakani akiwa amefukiwa akiwa amefariki"alifafanua Lutumo.

Kufuatia kifo cha mwanamke huyo, jeshi hilo linamsaka mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la ABDALLAH ambae ni mume wa marehemu kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mkewe .

Jeshi hilo pialimeendelea na msako wake na kufanikia kubaini matukio mengine ya uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...