SHIRIKA la Tanzania Health Support (THPS) limesajili watu 800 wakiwemo vijana wanaojidunga na dawa za kulevya nchini ili kuwapa elimu kuhusu madhara yanayotokana na dawa za kulevya.
Mkurugezi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt.Redempta Mbatia amesema watu hao wako katika hatari kubwa ya kupata virusi vya Ukimwi na kwamba wamesajiliwa ili kupatiwa elimu katika vituo vya Bagamoyo na Tumbi Mkoani Pwani.
Dkt.Mbatia amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Mkoani Lindi kuhusu shughuli zinazofanywa na THPS katika kusaidia serikali kutokomeza janga la ukimwi nchini ifikapo mwaka 2030.
"Lingine tunalolifanya katika kutokomeza janga la ukimwi ni kutoa huduma kwa wale wanaojidunga dawa za kulevya, watu hao wako katika hatari kubwa ya kupata maambuziki ya VVU, tunaendelea kuwaibua na kuwapa elimu endelevu ili waweze kuachana na dawa za kujidunga za kulevya," amesema.
Amesema watu hao wameingizwa kwenye clinic za methadone ambazo zinawasaidia kuachana na dawa za kulevya.
Akielezea shughuli nyingine ambazo zinafanywa na shirika hilo,amesema pia linafanya shughuli za kuwaibua waathirika wa VVU na kuwaanzishia dawa za kufubaza Virusi hivyo na kuwa na Afya yao nzuri.
Mkurungezi huyo amesema asilimia 97 ya wateja ambao wanahudumiwa na shirika hilo wameweza kufubaza VVU Kwa asilimia 98.
"Kumbukeni kuwa zile tisini na tano, lengo la tatu likiwa ni kufubaza angalau asilimia tisini na tano sisi tumeshafikia tisini na nane (98) kwa wale ambao Wana VVU tayari wameshafubaza," amesema.
Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Support (THPS) Dkt.Redempta Mbatia akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya (katikati) Dkt Godwin Mollel na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu) (kulia) George Simbachawene ambao walitembelea Banda la Shrika hilo katika maonesho ya shughuli za pambano dhidi ya Virusi ya UKIMWI nchini.
Maonesho hayo yamefanyika Mkoani Lindi ambapo pia maadhimisho ya Ukimwi duniani kitaifa yatafanyika leo ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi
Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la THPS Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kushoto) akizungumza na Balozi wa Marekeni Nchini Tanzania Dkt Donald Wright (katikati) ambaye alitembelea banda la THPS katika maonyesho ya shughuli ambazo zinafanywa na wadau mbalimbali Nchini katika kutokomeza Ulimwi nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...