Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania hivi karibuni alitangaza nafasi za ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), waliopo kwenye makambi na nje ya makambi wenye elimu ya kidato cha Nne, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya juu na Shahada kulingana na sifa zilizoainishwa katika tangazo hilo.

Sifa za Waombaji.
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b) Awe amehitimu mafunzo ya JKT/JKU

c) Awe amehitimu kidato cha nne kuanzia mwaka 2016 na kuendelea mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25.

d) Wahitimu wa Shahada, Stashahada ya juu na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.

e) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).

f) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa serikali.

g) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.

h) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.

i) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo)

j) Awe na urefu usiopunguwa futi tano(5.5) kwa wanaume, na futi tano inchi tatu (5’3”) kwa wanawake.

k) Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.

l) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.

m) Awe hajaajiriwa na taasisi nyingine ya serikali.

n) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.

o) Waombaji watakaofaulu usaili ndio watakaochaguliwa.

p) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa

q) Kwa mwenye elimu ya Astashahada, Stashahada, Stashahada ya juu na Shahada awe na fani zilizoainishwa kwenye (kiambatisho ‘A’).

Kama ilivyoelekezwa katika tangazo hilo, mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 27/12/2022. Kwa waombaji wahitimu wa kidato cha nne wenye sifa tajwa hapo juu waliopo Mkoa wa Mbeya walete maombi yao moja kwa moja ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest ya zamani barabara ya mahakama kuu kwa hatua zaidi za kiofisi.

Pia kwa mwananchi yeyote mwenye mashaka na mwenye uhitaji wa uelewa kuhusu tangazo hili afike ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kwa maelekezo zaidi.

Aidha nitoe rai kwa wazazi, walezi na vijana waombaji wa ajira hizi kuhakikisha wanafuata taratibu za uombaji wa ajira hizi ili kuepuka matapeli au wadanganyifu ambao wanaweza kuwalaghai kwa kuwataka kutoa kiasi fulani cha fedha.

Utaratibu wa kutuma Maombi.

i. Waombaji wote waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba zao za simu, kivuli cha kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA kwa ambao bado hawajapata kitambulisho, cheti cha kuzaliwa, cheti cha elimu ya kidato cha nne na cheti cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa anuani:-

Mkuu wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.

K.K
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
S.L.P 260
MBEYA.

Kwa maelezo zaidi niwatake waombaji wote kutembelea tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania www.policeforce.go.tz

Imetolewa na,
Benjamin E. Kuzaga,
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...