Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete akimtunuku Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Lojistiki na Usafirishaji Farida Salum katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika eo Desemba 16,2022 jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete (katikati) akiwa pamoja na viongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisimama kuimba wimbo wa Taifa katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika leo Desemba 16,2022 jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete akizungumza katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika leo Desemba 16,2022 jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete akisisitiza jambo kwa wahitimu wa kozi mbalimbali za Usafirishaji katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika leo Desemba 16,2022 jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali za Usafirishaji katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika leo Desemba 16,2022 jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa kozi mbalimbali za Usafirishaji wakiwa katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), yaliyofanyika leo Desemba 16,2022 jijini Dar es Salaam.

SERIKALI imesema inahitaji wataalamu wa kutosha, wenye weledi na chachu ya kukuza uchumi ili kusimamia miradi inayoendelea katika sekta ya uchukuzi.

Imesema imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, reli ya kisasa, meli na viwanja vya ndege hivyo, wataajiri wataalamu wazawa kuendeleza miradi hiyo.

Akizungumza leo Desemba 16, 2022 Dar es Salaam katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema anatambua changamoto iliyopo katika sekta ya ajira na kwamba itaendelea kuajiri wataalamu wazawa.

Amesema kuwepo kwa kozi mbalimbali za usafirishaji wa anga, meli, reli, maji na mabomba utaipunguzia serikali mzigo wa kugharamia mafunzo nje ya nchi ambayo hutolewa kwa gharama kubwa.


"Serikali inafahamu mahitaji ya chuo ikiwemo ukarabati wa majengo ya utawala na mabweni ya wanafunzi tutashirikiana kupata ufumbuzi endelevu wa kuboresha miundombinu hii lakini mnaweza kutumia mapato ya ndani kukarabati," amesema Mwakibete.


Pia amesema ndege mbili kwa ajili ya mafunzo ya urubani, injili moja na kifaa cha wahudumu wa ndege zipo njiani na kwamba serikali imetoa eneo katika uwanja wa JNIA kwa ajili ya mafunzo ya taaluma za usafiri wa anga ili kiandae wataalamu wa kutosha kwa ajili ya sekta ya uchukuzi na usafirishaji.


"Rai yangu chuo kitunze Vifaa hivi ambavyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa ili vitumike katika kupata mafunzo haya. Lakini pia niwaombe wahitimu wote msiridhike na utaalamu mliopata bali mtafute utaalamu wa juu zaidi ili taifa liweze kupata wataalamu wenye sifa zote zinazohitajika katika sekta," amesisitiza.

Mwakibete amesema ubunifu ni jambo muhimu kwa nchi kujenga uchumi imara na stahimilivu hivyo ni lazima wanafunzi waweze kuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha kuajiriwa au kujiajiri kwani taifa linahitaji nguvu kazi yenye maarifa na ujuzi zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zacharia Mganilwa amesema kwa sasa chuo kimeongeza udahili na kufikisha wanafunzi zaidi ya elfu kumi na mbili kwa mwaka 2022 ikilinganishwa na wanafunzi elfu sita kwa mwaka 2020.

Profesa Mganilwa ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kununua ndege mbili zenye injini moja kwa ajili ya shule ya usafiri wa anga zitakazosaidia wanafunzi wa urubani na uhandisi wa ndege.

Naye, Seif Gulamali, Mbunge wa Jimbo la Manonga mkoani Tabora na aliyewahi kuwa Rais wa wanafunzi wa Chuo hicho ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa bodi ya usafirishaji ili kuendeleza tasnia hiyo kwa kuzingatia weledi.

Katika Mahafali hayobn ya 38 jumla ya wanafunzi zaidi ya elfu mbili mia saba wametunukiwa shahada za uzamili, shahada, stashahada za juu, shahada na astashahada katika maeneo mbalimbali ya Usafirishaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...