Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Kikosi cha Simba SC kimesafiri kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) dhidi ya wenyeji Dodoma Jiji FC utakaopigwa Januari 22, 2023 kwenye uwanja wa Jamhuri jijini humo.

Kikosi hicho kimeondoka leo, Januari 20, 2023 kikiwa na Wachezaji 19 pekee, Benchi la ufundi na baadhi ya viongozi huku Wachezaji wengine wakiachwa jijini Dar es Salaam kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutumikia adhabu ya Kadi tatu za njano na wengine ni majeruhi.

Wachezaji wanne wametajwa kuwa na adhabu ya Kadi tatu za njano, Wachezaji hao ni Sadio Kanoute, Ousmane Sakho, Joash Onyango na Mzamiru Yassin wakati Wachezaji wengine wametajwa kuwa majeruhi, Wachezaji hao ni Moses Phiri, Peter Banda, Henock Inonga, Jonas Mkude na Clatous Chama.

Hata hivyo, kocha Juma Mgunda jioni ya leo amesema Chama hakwenda Dodoma kwa kuwa anaumwa na kwamba hata juzi alipotolewa hakuwa katika hali nzuri.

Kikosi hicho pia kimesafiri pia sanjari na Wachezaji wao wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili, Jean Baleke, Ismael Sawadogo na Mohammed Mussa.

Nini madhara ya kuwakosa Wachezaji hao kuelekea mchezo huo muhimu kwa upande wa Simba …? Hilo ndilo swali ambalo wengi wanajiuliza na jibu litapatikana baada ya mchezo wao na Dodoma Jiji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...