Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) kwa kushirikiana na Umoja na Ulaya wamewakutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuweka miongozo kuhusu bidhaa mpya ya hatifungani ya kijani ambay0 iko mbioni kuingia sokoni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana CPA Nicodemus Mkama amesema wamekutana na wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili kuleta bidhaa mpya ambazo zitasaidia kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Kama tunavyofahamu sasa hivi taifa letu linatekeleza mpango wa tatu wa maendeleo wa taifa ambao unahusisha miradi na kwa mantiki hii katika utekelezaji huo inahitajika kuwepo rasilimali fedha ili kutekeleza miradi, hivyo tunahitaji kuwa na vyanzo mbalimbali , hivyo tunatakiwa kuja na bidhaa tofauti katika masoko ya mitaji

“Sasa hivi hatifungani ambazo tunaita hatifungani za kijani ni mojawapo ya bidhaa ambazo zitatakiwa kuja kwenye soko letu la masoko ya mitaji na dhamana.Serikali kupitia Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya…

“Tumekuja na mkakati wa kuweka miongozo itakayosaidia kupata vyanzo hivi ambavyo vitatoka katika uwekezaji mbalimbali hapa Tanzania lakini pia na wawekezaji wa kimataifa.Kwa mantiki hiyo leo tunao wawezeshaji ambao wanatoka Umoja wa Ulaya ili kushirikiana na Mamlaka yetu kuhakikisha tunawajengea uwezo wadau wetu,”amesema .

Mkama ameongeza lengo ni kuweka mazingira wezeshi ya kupata bidhaa hizo ambazo zitatumika katika kugharamia miradi mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi huku akifafanua bidhaa ya kijani ni mpya katika soko la Tanzania na mpaka sasa haijatolewa katika soko, hivyo wanaweka miongozo itakayowezesha kutoa hatifungani hiyo.

“Mpaka sasa tumetoa hatifungani ambazo zinakuwa na matokeo chanya katika jamii yetu , katika mwaka huu tumeidhinisha hatifungani inayoitwa Jasiri iliyotolewa na Benki ya NMB na hatifungani hii ilikuwa na matokeo mazuri ya kuleta muamko mkubwa katika sekta ya fedha.

“Kwa mantiki hii kuna uhitaji mkubwa wa kuleta bidhaa mpya na mojawapo ya bidhaa hizi ni hatifungani ya kijani ambazo ni bidhaa zinazowezesha kuvutia wawekezaji wa kimataifa ambao wanataka kuwekeza katika kulinda mazingira.Kwa hiyo fedha zitakazopatikana zitakwenda kutekeleza miradi kama kuwa na miradi ya mabasi ya mwendokasi yenye mfumo wa kulinda mazingira.

“Lakini tunaweza kuwa na vyanzo mbadala kama miradi itakayotumia gesi asilia ili kujenga misitu yetu, kwa hizi hatifungani za kijani ni mojawapo ya hatifungani za bidhaa zinazotumika kimataifa kupata fedha zinazotumika pia kutekeleza miradi ya maendeleo.”


OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama akizungumza jambo mbele ya kikao kazi cha wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili kuleta bidhaa mpya ambazo zitasaidia kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo,Kikao kazi hicho kimefanya Januari 24,2023 jijini Dar es salaam.







Wadau wa kikao kazi hicho wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo

OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama akiwasilisha mawasilisho mbalimbali kuhusu MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA)




Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Mahusiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw. Cedric Merel akifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama (hayupo pichani) kwenye kikao kazi hicho.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Mahusiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw. Cedric Merel akizungumza jambo mbele ya Washiriki wa Kikao kazi hicho cha wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili kuleta bidhaa mpya ambazo zitasaidia kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Mahusiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw. Cedric Merel akifurahia jambo na OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama wakati wa kikao kazi hicho.




















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...