Na Khadija Seif , Michuzi TV


FAINALI ya Msimu wa 13 wa Shindano la Bongo Star Search (BSS) zinatarajiwa kufanyika Februari 4,2023 huku Mshindi wa kwanza akitarajiwa kuondoka na kitita cha fedha Sh.milioni 20 .

Akizungumza leo Januari 24,2023 , Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark 360 ambaye pia ndio Jaji Mkuu wa Shindano la BSS Ritha Paulsen maarufu Madame Ritha amesema wamekuwa na msimu 12 lakini msimu huu wa 13 umekuwa wa kitofauti zaidi na misimu yote kwani washiriki wamepata nafasi ya kazi zao kuwepo kwenye ntandao wa kimataifa wa kupakua nyimbo wa Boomplay.

Amefafanua kwamba mshindi wa kwanza atapata fedha Sh. Milioni 20, mshindi wa pili Sh. Milioni tatu na mshindi wa tatu ni Sh. Milioni moja licha ya zawadi hizo tayari washiriki nane wamepata nafasi ya kurekodi nyimbo zao na kufanya video kwa watayarishaji nguli na wabobezi.

Akielezea zaidi amesema Msimu huu ni wa tofauti na haijawahi kutokea kwani kulikuwa na majaji ambao ni mastaa wakubwa akiwemo Rayvan,Nandy, Jux na wengine wakali ambapo walifanya mchujo wa hali ya Kuu bila upendeleo kwa kuchagua vipaji vyenye kustahili kuingia 10 bora,"amesema na kuongeza mashabiki wa muziki mzuri washuhudie vipaji vipya na kwa kushirikiana na Boomplay.

Amesema msimu huu ulikuwa wa kuwapatia mashabiki ladha mpya, kuwajenga na kuwawezesha vijana kuwa mastaa kwa kuwa na nyimbo zao wenyewe huku kunufaika na kazi zao wakianzia nafasi waliopo ili kuwajengea nafasi ya kufanya kazi za muziki kama sehemu ya ajira sio kipaji peke yake.

"Haya yote ndio tumefanya msimu huu kuwa wa tofauti sana na misimu mingine yote, msimu huu tulikuwa na wadau wengi sana wa muziki ambao tumekaa nao na kushirikiana kufanikisha jambo hilo pamoja na wadhamini wenye nia ya dhati ya kuhakikisha vipaji hivi vinapewa nafasi."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kwa namna ambavyo wanaunga mkono vijana kwa kuhakikisha kuna programu nyingi na kuongeza wanatambua juhudi za Serikali chini ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA,) za kukuza sanaa ya muziki kwa vijana.

Pia amesema Startimes imekua ikishirikiana na Benchmark production kwa kipindi kirefu kuvumbua vipaji vya muziki vilivyojificha na kuhakikisha vinatambulika kwa umma na kufika."Kampuni ya Startimes chaneli ya ST Swahili imekua ikionyesha mashindano haya kwa uzuri na weledi mkubwa.

"Safari hii ni kali sana na balaa zaidi ni fainali ya Februari 04,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam niwaombe watazamaji kuhakikisha wanalipia visimbuzi vyao kuona faina hizi au kwa wale ambao wana simu janja wanaweza kuona burudani hii kupitia mtandaoni kwenye Startimes on."

Ametoa rai kwa kampuni na wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada za jukwaa hilo kuhakikisha ndoto za vijan wengi wenye vipaji zinatimia.
Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Januari 24,2023 ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam mara baada ya kutangazwa tarehe rasmi ya fainali ya shindano la bongo star search Msimu 13 (All Star).
Mkurugenzi wa Benchmark production Ritha Paulsen akizungumza na Wanahabari Leo Januari 24,2023 pamoja na baadhi ya wadhamini  kushoto kwake Mkurugenzi wa Kampuni ya Startimes David Malisa kulia kwake Mmiliki wa kumbi za starehe ambao utafanyika fainali ya Bongo star search  ukumbi wa Superdome   Scott Farrell akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye fainali hizo Februari 4,2023 katika ukumbi huo Jiji Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...