*Asema wanaochezea fedha za serikali wajue wanacheza na moto

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Gairo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameziagiza Mamlaka za Serikali mbalimbali kuhakikisha zinasimamia vema fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kufanya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundimbinu ya barabara huku akieleza kucheza na fedha za umma ni sawa na kucheza na moto.

Chongolo ameyasema hay oleo Januari 28 mwaka 2023 wakati anazungmza na wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa barabara inayotoka kwenye wilaya hiyo hadi Iringa ambayo ujenzi wake unandelea na changamoto kubwa ikiwa ujenzi wa madaraja ambayo yamechangia kuchelewesha kukamilika kwa ujenzi.

“Niagize Mamlaka za Serikali mbalimbali ikiwemo za Mkoa huu wa Morogoro miundombinu mbalimbali iliyojengwa inatumia fedha nyingi ambazo zinatokana na kodi za wananchi lazima zisimamiwe ili kuleta matokeo.Kama daraja hili lingesimamiwa vizuri mwanzo kwa ubora leo tusingekuwa na mjadala wa kujadili daraja tungekuwa tunajadili mambo mengine ya maendeleo.

“Iwe fundisho na mara ya mwisho viongozi ambao wanapewa jukumu la kusimamia maeneo wahakikikishe wanatimiza wajibu wao wa kusimamia ubora wa kazi zinazofanywa kwenye maeneo husika, thamani ya fedha kwenye miradi husika ionekane.Mambo ya kucheza na fedha za umma ni kucheza na moto , tusiruhusu watu wa namna hiyo kuchezea fedha kwasababu wanakwamisha  maendeleo yetu wenyewe,”amesema Chongolo.

Awali wakati akizungumza na wananchi Chongolo amesema amefika kwa ajili ya kuangalia changamoto mbalimbali na wakati anaanza ziarake alizungumza na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amemuagiza kupita kuangalia changamoto ya madaraja pamoja na barabara, vituo vya afya, zahanati, pamoja na maeneo mbalimbali.

“Mwenyekiti wa Chama chetu na Rais ameniambia nihakikishe naangalia  barabara inayoanzia Gairo kwenda Iringa nione changamoto ya madaraja na nione nini kinachoendelea.Nimekuja kwa maelekezo yake  mwenyewe, nimeona changamoto iliyopo  na nimepita ,nimeishuhudia.

“Nimshukuru  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa namna anavyohangaika kufuatilia utatuzi wa changamoto, ameeleza hatua alizokwisha chukua na viongozi wa Wizara ya Ujenzi waliofika hapa kwa idadi yao.Sasa hivi hatuna ile ya kuambiana ahadi ahadi, sasa ni lazima ni utekelezaji, tayari Rais alishatoa zaidi ya Sh.bilioni 100 kwa ajili ya kuchora michoro ya namna daraja litakavyopita.

“Kuangalia vifaa vitakavyotumika kujenga lakini wakati wa kuchora ndio unakadiria na gharama ya ujenzi na haikufanyika kwa daraja moja, imefanyika kwa daraja la Matale, daraja la Chakwale kwa maana ya kwamba ili barabara hii ikamilike, ipitike ukijenga daraja hili moja hutaweza kuwa umeifungua kwa maana hiyo lazima ujenge daraja la Ruyami, Chakwele na Matale.”

Chongolo amesema kwenye upande wa utengenezaji barabara na ushindiliaji mambo mazuri lakini changamoto ipo kwenye madaraja matatu na kwasababu, hivyo amewahakikisha  ameona na anakwenda kwa Rais kumueleza ili aone jinsi ya kuitatua, wananchi wanasubiri madaraja.

“Hapa lilishawahi kujengwa daraja lakini likakatwa na maji kutokana na  kutokuwa na ubora , hivyo sitaacha daraja lingine lijengwe halafu tuanze kupigiana hadithi , kwa hiyo fedha zitakapopatikana name nitakuwa sehemu ya wasimamizi wa daraja hili,”amesema Chongolo huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi wa Gairo kwa kujituma kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo.





Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ukikatisha  kando ya daraja la Mto Nguyami mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Mkwajuni na Ilalo  na kujionea kero kubwa ya kukosekana kwa daraja katika mto Nguyami linalounganisha vijiji hivyo viwili wilayani Gairo mkoa wa Morogoro,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...