Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 32 bora michuano ya Kombe la Azam Sport Federation ASFC utakaopigwa saa 16:00 jioni dhidi ya Copco FC ya Jijini Mwanza inayoshiriki Ligi ya Championiship .

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi yake ya mwisho mapema leo asubuhi ikiwa ni mara baada ya kutoka kupoteza mchezo wa Ligi kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Namungo na kwamba kikosi kipo tayari kwa mchezo huo hapo kesho.

KMC FC imeingia katika hatua hiyo ya 32 bora ikiwa ni baada ya kuifunga Timu ya Tunduru Korosho magoli sita kwa moja mchezo uliofanyika Disemba 11 mwaka jana kwenye uwanja wa Uhuru Jijini hapa huku mshambuliaji Sadalah Lipangile akifunga Hatriki.

“ Tunakwenda kwenye mchezo ambao tunafahamu kabisa kwamba ukipoteza utakuwa umeaga michuano hiyo, lakini kama KMC FC malengo yetu ni kwenda kufanya vizuri ili tusonge mbele zaidi jambo ambalo linawezekana kwasababu siku zote Timu bora huwa haipotezi mchezo mara mbili.

Michuano ya ASFC ni muhimu kwetu na tunaichukulia kwa ukubwa wa namna yeke, jambo ambalo hata kwenye mazoezi wachezaji wameonesha nia na uhitaji wakufanya vizuri , lakini pia kupitia mchezo huo tutautumia kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu mwingine wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting ambao utachezwa Februari tano mwaka huu.

Katika mchezo wa kesho, tunakwenda tukiwaheshimu wapinzani wetu kwa sababu siku zote hakuna mchezo mwepesi wala Timu nyepesi, haijalishi inashiriki ligi gani ama ipo kwenye nafasi gani, hivyo tunawakaribisha sana Copco kwenye Manispaa yetu ya Kinondoni”.

Aidha kuhusu Afya za wachezaji wote wapo vizuri na kwamba kila mmoja amejiandaa vema kuhakikisha Timu inapata matokeo mazuri na kuendelea kwenye hatua inayofuata, mashabiki wa KMC FC wajitokeze kwa wingi kuwasapoti vijana wetu hapo kesho pindi watakapokuwa uwanjani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...