Na Mwamvua Mwinyi, Pwani


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Fadhil Maganya ametoa rai kwa wanachama na viongozi wa Jumuiya hiyo kuhamasika kuanza kujenga ofisi za kisasa kwa ngazi zote ili kuimarisha Jumuiya.

Aidha amewaasa kuhakikisha wanabuni vyanzo vya kiuchumi, miradi ya kujiendeleza ili Jumuiya na Chama iwe na misuli kiuchumi.

Akizungumza na viongozi wa Jumuiya mbalimbali na chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Pwani, baada ya kupokelewa kwa ajili ya ziara yake ya kwanza tangu achaguliwe,Maganya alisema yupo Mkoani humo kwa kazi maalum, kwa sherehe ya miaka 46 ya CCM ambapo kilele chake ni februari 5 mwaka huu.

"Tunakumbushwa kuweka makazi yetu ya chama,tuhamasike kujenga ofisi zetu kwanii hii ni kazi yetu sote'

Vilevile "Tuonyeshe tunakuja kisasa ili chama chetu kiwe na misuli ya kiuchumi kwa kuimarika kiuchumi na kisiasa"anasisitiza.

Aidha alieleza ,wanachama wanapaswa kuhamasika kujisajili kielektroniki na kushawishi wanachama wapya .

"Wanatakiwa wanachama wahamasike kujisajili kielektroniki,na washawishi wanachama wapya "alisisitiza Maganya.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ?Mkoa Jackson Josiah Kituka, alieleza tathmini ya Jumuiya na kueleza katika uchaguzi mkuu uliopita wameshinda maeneo yote kasoro kata moja ambapo ameahidi ushindi kwa vitongoji vyote kwenye uchaguzi wa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake UWT mkoa Zainab Vullu alimtaka Mwenyekiti wa wazazi Taifa kumpelekea salama Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa aondoe hofu kwa mkoa wa Pwani,kwani upo salama na uchaguzi 2024 na 2025 watashinda kwa kishindo.

"Tupo salama, hatuna mashaka, wanawake jeshi kubwa na Tutahakikisha Rais Samia 2025 anashinda "alisema Vullu.

Katika ziara hiyo ,Maganya amekagua na kutembelea jengo la dharura hospital ya wilaya Msoga Chalinze,kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupanda mti kati ya miti 151 itakayopandwa hospitalini hapo, kushiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi Bwilingu na kuongea na wananchi Bwilingu, Januari 28 atakuwa wilayani Rufiji ikiwa ni maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.##

Picha mbalimbali za ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Fadhil Maganya...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...