John Walter-Manyara.

Kampuni ya Mati Super Brands Limited imecheza mechi ya kirafiki na kampuni ya Bonite bottlers ltd katika uwanja wa Kwaraa Mjini Babati mkoani Manyara ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza vipaji vya soka pamoja na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa kampuni hizo zinazozalisha vinywaji aina mbili tofauti.

Mati super Brands Ltd wao wanazalisha vinywaji aina ya pombe Kali huku Bonite wakitengeneza vinjwaji baridi.

Kampuni hizo zote zipo mbele katika masuala mbali mbali ya kijamii na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Manyara na taifa kwa ujumla.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Elvis Peter amesema kuwa mechi hiyo ni muendelezo wa kampuni hiyo kushirikiana na makampuni yaliyoko mkoani hapa pamoja na kujenga ujirani mwema.

Elvis ameupongeza uongozi wa Mati Super Brands Limited pamoja na Bonite Bottlers ltd kwa kutoa fursa kwa wafanyakazi wao kushiriki katika michezo ya pamoja ambayo inasaidia kukuza vipaji na kuimarisha afya za miili yao ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuzalisha kwa tija.

Nahodha wa Timu ya Bonite Bottlers limited Maboya Ramadhan amesema amefurahishwa na mchezo huo ambao uligubikwa na ushindani mkubwa ,na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano na kuhimiza michezo kwa wafanyakazi.

Maboya ameendelea kusema kuwa Bonite wamekua mstari wa mbele katika kuibua vipaji vya soka kwa vijana na kutoa fursa kwa vijana kujiendeleza kimichezo.

Katika mchezo huo Mati Super Brands Ltd ilibamizwa mabao 3-0 huku mkurugenzi wa kampuni ya Mati Super Brands David Mulokozi akishuhudia Dakika 90 za mchezo huo ambao utarudiwa siku yeyote Kwa mujibu wa Kocha Elvis Peter akieleza kwamba hawajaridhishwa na matokeo hayo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...