MIAKA 20 ya Onyesho la Ubunifu Wa Mavazi lijulikanalo Kama Lady In Red Kufanyika Februari 11 Jijini Dar es Salaam onyesho hilo kujumuisha kwa urahisi kwa kutoa mfululizo wa kujionea ubunifu mbalimbali wa mavazi ambao huonyesha ushirikishwaji na kuangazia wabunifu na wanamitindo wenye ulemavu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hugo Domingo, Mario Fernandes akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alisema kuwa Mitindo huwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwapa jukwaa ambalo litawajengea Imani, uwezo na kutoa fursa kuonyesha vipaji vyao.

Amesema Onyesho la Mitindo la Lady In Red, limeonyesha utofauti wa asili na wa ndani mikusanyiko ya wanaume na wanawake kutoka kwa wabunifu wa mavazi.

Aliongeza “Mwaka huu, tunafuraha kwa onyesho hili, kwani limeunda fursa zaidi kwa wafanyabiashara wa ndani na wabunifu, tulifanya hafla ya kutambulisha uwepo wa Lady in Red mwaka huu kwa kushirikiana na Neekofoods - Tukio ambalo lilikutanisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma ya Chakula ambapo moja kwa moja waliweza Kufurahia chakula kizuri huku wakijionea maonyesho ya ubunifu wa mavazi ambapo tukio hili liwakutanisha pia ma-DJ wajao, vipaji vipya na lengo kubwa ni kuhamasisha tukio hili maarufu la mitindo litakalofanyika tarehe 11 Februari 2023 katika eneo ukumbi maarufu Warehouse zamani ( Next Door Arena) Ambapo leo Januari 28, 2023 tumefanya usaili wa kuchagua Model's kwaajili ya onesho hilo siku hiyo ya Februari.

.

Hugo Domingo kwa miaka miwili na ndiye muaandaji mkuu wa onyesho letu la Lady In Red mwaka jana tulikuwa na maoni chanya, onyesho la mavazi lilikuwa na wabunifu ambao walikubali kutumia utajiri wao Wa sanaa na utamaduni wa Kitanzania. ili kuongeza thamani kwa wageni wetu tulikuwa na safu ya shughuli ikijumuisha uwepo wa safu mbalimbali za MaDJ za moja kwa moja, maonyesho ya moja kwa moja na tafrija ya kufurahisha baada ya hafla katika klabu maarufu ya Elements.” alieleza

Kwa Upande Meneja wa Mradi wa Lady In Red Fashion Show, Harith Juma alieleza kuwa “Mwaka huu tuna wabunifu wapya wengi na wa kutosha wakati huu wakiwemo wabunifu wapya na wenye vipaji 12 ambao walichaguliwa na Chama cha Mitindo Tanzania. Tunatarajia ubunifu mzuri kutoka kwa Joyce Kibaja , Nally Boutiques, BK Brands , Volla Attire , QB Atelier , Fiderines House of Catwalks & Fashion, MK Nuru Designs , Kasikana , Joe Designs , Culture ,3 in 1 Attire , na Diana Komba Designs.".

Mkurugenzi wa Ubunifu wa onyesho hilo Osbert Fernandes alisema “Onyesho Hilo litawekwa mandhari nzuri na litakuwa la aina yake, na kwa mara ya kwanza Tanzania, tunatarajia kutoa onyesho bora kwa wageni wetu, na tunatarajia kuona watu wengi wanakuja kusherehekea. Miaka 20 ya onyesho la Lady In Red Fashion kuanzia saa 7 mchana, kwa hivyo hakikisha unapata tiketi yako mapema mwaka huu na tunakuahidi show nzuri siku hiyo.”

Harith Juma alisisitiza "Tunahitaji watu kuja kuunga mkono onyesho hili, kwani sio tu itakuwa usiku mzuri wa kusherehekea mitindo, na usiku mzuri wa kupumzika na familia na marafiki, lakini onyesho letu pia linarudisha kwa jamii, kwa asilimia ya faida itatengwa kusaidia mahitaji kwa ajili nyumba ya Tushikamane inayowasaidia wazee. Tiketi zinapatikana kwa viti mbalimbali vya kawaida TZS 50,000 na VIP 100,000 TZS, wote wanaopenda wanaweza kununua kupitia Nilipe, Warehouse lounge & Bar, Ally Rhemtula Store Masaki, Hugo Domingo Offices na ofisi za Black fox.

Miaka ya hivi karibuni Asya Idarous alianzisha ushirikiano na kampuni ya Hugo Domingo Limited, kampuni maarufu ya upambaji yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam ikiwa na Ofisi pia Arusha, Dodoma, Mwanza, Zanzibar na ikiwa na Mahusiano pia na nchi mbalimbali za Afrika.

Kwa zaidi ya miaka 20, onyesho la mitindo la Lady In Red limetumika kama jukwaa la kizazi kipya cha mitindo, Lady in Red imeanzishwa na Asya Idarous Khamsin mnamo mwaka 2003, alianzisha Maonyesho haya ya mitindo na limewakuza wabunifu wa mitindo mbalimbali kama vile Ally Rhemtula, Miriam Odemba, Khadija Mwanamboka, Mustafa Hassanali, Martin Kadinda, Flaviana Matata, Ria Fernandes, Victoria Martin na wengine wengi.

Shukurani zimetolewa kwa wadhamini na washirika wote wakiwemo Benki ya CRDB Plc, Mapinduzi, Wasafi Media , Asya Khamsin , Image masters Limited , Aquasoundstz , Event masters Tanzania , MMI Tanzania , Niya Beauty , Tridea Cosmetics , Blackfox models , 361 Tanzania , Martin Kadinda , Ally Rhemtulla , LAS Consultancy , Rhythm Africa , Neekofoods , Elite Tanzania , African Star , Istudio , Dar Life , Infocus Studio , Warehouse Tanzania, BASATA , Kavs group and Fashion Association Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...