Na Muhidin Amri,Namtumbo

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas, amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuendelea kupanda miti katika maeneo yao ili kurudisha uoto wa asili utakaosaidia mkoa huo kuwa na uhakika wa kupata mvua mara kwa mara.

Laban Thomas, ametoa wito huo jana wakati akikabidhi miche ya miti ya matunda na mbao kwa viongozi wa kwaya ya mahakama kuu kanda ya Songea kwenye viwanja vya jengo la mahakama ya wilaya ya Namtumbo.

Alisema,ni muhimu kwa wananchi na taasisi za serikali mkoani Ruvuma,kuhakikisha wanaendelea na utamaduni wa kutunza mazingira kwa kuanzisha vitalu vya uoteshaji miche ya miti kama sera ya Taifa inavyosema.

Ameziagiza,serikali za vijiji,kata na wilaya kuhakikisha wanachukua hatua na kutumia sheria ndogo kudhibiti uharibifu wa mazingira katika maeneo yao ikiwamo kudhibiti uingiaji wa wafugaji na mifugo,badala ya kusubiri hadi pale hali inatakapokuwa mbaya.

Mkazi wa mtaa wa Minazini Namtumbo mjini Ali Ndauka,ameiomba serikali ngazi ya wilaya na mkoa kuchukua tahadhari ya kudhibiti uingizaji wa mifugo usiozingatia sheria kwenye baadhi ya vijiji wilayani humo.

Ndauka alisema,kama serikali haitachukua hatua madhubuti kukabiliana na vitendo hivyo basi kuna hatari kubwa ya wilaya ya Namtumbo na mkoa wa Ruvuma ambao bado una rasilimali kubwa ya ardhi na misuti kugeuka jangwa.

Alisema, baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji wamekuwa sehemu ya kuingia kwa wafugaji na mifugo yao wasiofuata taratibu kutokana na tamaa ya kupata fedha jambo linalo hatarisha wilaya ya Namtumbo kutokea kwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji.

Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa hapa nchini,inayotajwa kuwa na kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji miti ovyo na uingizaji mifugo holela, hivyo kutishia mkoa huo unaotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kugeuka jangwa kwa siku za baadaye.
Jaji Kiongozi wa Mahakama kuu  ya Tanzania Mustapha Siyani akimwagilia maji mti wa kivuli kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma,kushoto Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Songea Dkt Yose Mlyambina.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas wa tatu kushoto,akikabidhi miche ya miti kwa viongozi wa kwaya ya Mahakama Kuu kanda ya Songea kulia, kwenye viwanja vya jengo la mahakama ya wilaya Namtumbo mkoani humo,wa pili kushoto Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu na wa kwanza kushoto Mkuu wa wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Wakili Julius Mtatiro kulia,akimsikiliza mtendaji wa Mahakama ya Tanzania Richard Mbemba ambaye  aliwahi kuwa katibu tawala wa wilaya ya Tunduru walipokutana kwenye ufunguzi wa jengo la mahakama ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...