Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu ametoa pongezi kwa Jumuiya ya Wazazi ya mkoa huo kwa kuandaa mafunzo maalumu ya uongozi kwa ajili ya viongozi wake huku akitumia nafasi hiyo kueleza masuala mbalimbali kwa mustakabali wa Chama hicho ngazi ya mkoa.

Pamoja na pongezi hizo kwa Jumuiya ya Wazazi inayoongozwa na Mwenyekiti wake Hadija Ally Mtemvu amesema katika mambo ambayo hataki kuona yanafanyika katika uongozi wake ni vitendo vya rushwa na uonevu.

Mtevu ameyasema hayo leo Januari 12 ,mwaka 2023 wakati akifungua mafunzo ya uongozi yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa moja ya maazimio ya mkutano mkuu wake ambao ulitokana na azimio la kuandaliwa kwa mafunzo kwa ajili ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa jumuiya hiyo ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Akizungumza mbele ya washiriki wa mafunzo hayo , Mwenyekiti Mtevu pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa CCM Mkoa wa Dar es Salaam haitakuwa tayari kuona viongozi wakijihusisha na vitendo cha rushwa ili kutoa upendeleo kwa wanaowania nafasi za uongozi.

“Sitaki kusikia rushwa , nimekuwa kieleza kwa kamati ya siasa katika adhabu kubwa ambayo nitaitoa ni pale nitaposikia mtu amepokea rushwa ili kumsaidia mtu mwingine apate uongozi.Tunataka mtu mwenye uwezo apewe nafasi na asiye na uwezo asipewe.Tukibaini hilo litakuwa ni kosa kubwa.

Aidha amesema katika uongozi wake hataki mambo ya uonevu kwasababu yeye mwenyewe amepitia machungu hayo huku akieleza anataka kuona CCM Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2024 washinde kwenye nafasi zote na hiyo itatokana na kuweka watu wenye sifa ya uongozi ambao watakubalika kwa wananchi.

“Pia mwaka 2025 tunataka madiwani wetu washinde kwa kishindo , tunataka Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan mwaka 2025 kwa Dar es Salaam apate kura za kutisha , lazima tumuandalie watu ambao watakuwa na uwezo wa kufanya kampeni sio kuwa na watu ambao wenyewe kupata nafasi ni kashehe.

Pia Mtevu amesema kama kuna mtu ameingia ndani ya CCM kwa lengo lake yeye akipata taarifa atamfukuza halafu akienda mbele naye atakwenda mbele wakae kwenye meza wabishane na hao wakubwa lakini kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam wahawataki mchezo.“Kama umeingia kwa malengo yako katika miaka mitano hii usitarajie.”

Aidha ametumia nafasi hiyo kumshukuru kiongozi wa Jumuiya ya Wazazi kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatasaidia katika mambo mengi katika mkoa wao wa Dar es Salaam na huenda ndio wa kwanza kuandaa mafunzo hayo ya uongozi.

Kwa waliochaguliwa amewataka wamshukuru Mungu na wamtangulize Mungu na pili watambue kuwepo kwao hapo ni kwasababu CCM ilitaka wawepo.“Kwa hiyo haya yote mawili muyajue katika kazi zenu za kila siku, na tatu ni vizuri kujua wanachama walikuwa na imani na ninyi ndio maana walikuchagua , kwa hiyo utakuwa unamtanguliza Mungu mbele, Chama chako na waliokuchagua, tukifanya hivi kila jambo litakwenda vizuri zaidi.

Aidha amesema jambo kubwa na muhimu viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam watambue Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anaimani na timu yote iliyochaguliwa katika kipindi hiki , hivyo wana kazi kubwa ya kuifanya ili kumdhirihishia hakuingia kimakosa.

“Tupo kwasababu ya kuhakikisha Chama kipo imara na ushindi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 unapatikana kwa kishindo na mwaka 2025 tunamchagua Dk.Samia dk. kwa kura nyingi sio za kubahatisha , ninawaomba ninyi muwe sehemu ya kiungo kwa wazazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa wananchi wote wa mkoa huo.”

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally ameeleza sababu za msingi ambazo zimewasukuma kuandaa mafunzo hayo ya uongozi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali za jumuiya hiyo ambapo amesema kweli wameingia kwenye baraza lakini inawezekana wametoka kule chini wakiwa, ushabikiki na mapenzi ya dhati ya Chama chao kuja kukihudumia lakini hawajui mipaka yao.

“Hatujui mipaka yetu, hatujui nini maana ya kuwa kiongozi, lakini hatujui nini maana ya haiba ya uongozi hatujui maadili ya uongozi , kwa hiyo Chama Cha Mapinduzi ni tanuru ambalo linatengeneza viongozi , makini na mahiri kwa hiyo tumechukua azimio la mkutano mkuu wa juuiya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanza na Kamati ya Utekelezaji,”amesema Hadija Ally.

Amemhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwamba mafunzo hayo ya siku tatu yanayoanza na kamati ya utekelezaji Mkoa wa huo yatafanyika katika ngazi zote ili kuhakikisha viongozi wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu uongozi.“Nia na madhumuni ni kuwa na viongozi sahihi ambao watakaa katika jamii yetu na kuweza kuhakikisha chama chetu kinashinda uchaguzi mkuu mwaka 2025.”
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Abbas Mtemvu akifungua mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo Januari 12,2023 katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam,pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally na kushoto ni Katibu wa Organization ya Wazazi CCM Taifa Bw.Saidi King’eng’ena
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Abbas Mtemvu katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo Januari 12,2023 katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Organization ya Wazazi CCM Taifa Bw.Said King’eng’ena akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.







Baadhi ya Wanakamati wa Jumuiya hiyo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo

Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Adam Ngallawa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.








Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akiwa picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Utekelezaji katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi hao yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Abbas Mtemvu akipokewa na Mwenyekiti wa Wazazi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally mara baada ya kuwasili leo Januari 12,2023 katika hotel ya Star Breeze iliyopo Mbutu Kigamboni kwa ajili ya kufungua mafunzo ya Uongozi kwa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...