SERIKALI imezindua shule jumuishi ya Msingi ya kwanza ya mfano nchini kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini.

Shule hiyo ya Lukuledi iliyopo katika wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara imezinduliwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda.

Amesema shule hiyo imejengwa na Wizara hiyo kupitia mradi wa kuendeleza ujuzi nchini (ESPJ).

"Shule hii ya Jumuishi ya Msingi ni ya kwanza ya mfano ambayo huwezi kuiona sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania kwa usawa, wingi wa miundominu na kutoa mahitaji yote kwa wanafunzi wote wenye mahitaji maalumu," amesema.

Profesa Mkenda amesema shule hiyo haina mfano Tanzania nzima ina miundominu ya Kutosha kukidhi mahita yote ya watoe wenye mahitaji maalumu.

Ametaja baadhi ya miundombinu hiyo kuwa ni mabweni yenye vyumba maalum vya kipekee (self-contained) kwa wanafunzi wenye ulemavu wa viungo ambao wanatumia wheelchairs.

Miundombinu mingine Maalumu kwenye shule hiyo ni chumba Maalumu kwa ajili ya kupima usikivu kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Shule hiyi pia ina karakana sita ikiwemo karakana ya magari, ushonaji , saluni kwa ajili ya kutoa Mafunzo stadi kwa wanafunzi.

Amesema ujenzi wa shule hiyo ambayo imegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja ni kutokana na juhudi za Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu waandikishwa, wanafundishwa na kupata elimu kukamilifu.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu Katika wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda (kulia) akizindua shule ya Jumuishi ya Msingi ya Mfano ya kwanza kujengwa nchini kwa ajili ya kutoa Elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini.

Muonekano wa shule Jumuishi ya Msingi ya Mfano ambayo imejengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watoto wenye mahitaji maalumu nchini. Shule hiyo ni ya kwanza nchini ambayo ina miundombinu yote muhimu kwa ajili ya kutoa mahitaji maalumu Kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...