Na Mwandishi Wetu

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) imepongeza maendeleo ya utekelezaji ujenzi  mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115 uliofikia asilimia 81.82 hadi kufikia Januari 31, 2023.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA, Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa ziara ya kutembelea  mradi wa Julius Nyerere ikiwa ni kitekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia  Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizindua  ujazaji maji kwenye bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

"Mhe. Rais alituagiza sisi DAWASA tunufaike kupitia maji ya mto Rufiji kwa kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani baada ya kuwa yamezalisha umeme,"amesema Jenerali Mwamunyange.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amepongeza kazi nzuri iliyofanyika kwenye mradi huo  na amefurahi  ushirikiano  mkubwa uliopo kati yao (DAWASA) na TANESCO

Awali Mhandisi Mkazi Lutengano Mwandambo alieleza kuwa zoezi la ujazaji maji linaendelea vizuri na limefikia mita za  ujazo 131.02 kutoka usawa wa bahari.






Matukio mbalimbali katika picha wakati Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA ilipotembelea mradi wa kimkakati wa Julius Nyerere -JNHPP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...