Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA ya hakimu Mkazi kisutu imemuachia huru Mkazi wa Mbweni Dar es Salaam, Boi Rajabu (60) aliyekuwa akikabiliwa na kosa moja la mauaji kwa kutumia kisu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 23, 2023 mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya aliyekasimiwa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mbuya amesema, hakuna shahidi yeyote kati ya mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi walioweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa Boi ndio aliua.

"Upande wa mashtaka ulileta mashahidi sita na vielezo vitatu ambavyo ni taarifa ya uchunguzi wa kifo,ramani ya tukio, na onyo la polisi lakini katika mashahidi walioletwa hakuna ushahidi wa mtu aliemuona Mzee boi Rajabu akimchoma kisu marehemu ila wote waliambiwa na ndugu wa marehemu alifahamika Kwa jina la Adam Matitu ambaye hakufika mahakamani hapa kutoa ushahidi wake" amesema Hakimu Mbuya.

Ameongeza kuwa, mashahidi katika ushahidi wao walidai kuwa Matitu ndie Alie waambia kwamba marehemu alichomwa kisu na mshtakiwa Boi ambapo walidai Matitu aliwaambia kuwa aliambiwa na marehemu kabla hajafa.

Mbuya alidai kuwa Mtuhumiwa alihusishwa na mashtaka hayo tu baada ya kutajwa na Adamu Matitu ambaye upande wa mashtaka umeshindwa kumleta kwaajiri ya kithibitisha kwamba aliambiwa na marehemu kuwa Boi ndiye anayehusika na kifo chake.

Aliongeza kuwa, ushahidi pekee unaomuhusisha mshitakiwa na kesi hiyo ni kielellezo Cha onyo ambapo shahidi namba sita coplo Erasto alidai amekiri mbele yake ambao nayo wakati shahidi anatoa maelezo hayo alikumbana na pingamizi kwamba mtuhumiwa hakuwai kuandika maelezo polisi.

"Kanuni inasema endapo mahakama itaamua kuegemea upande wa ushahidi wa maelezo yaliyokataliwa basi mahakama itapaswa kujihoji Juu ya hatari itakayotokea na kama maelezo hayo yatakuwa ni ya ukweli basi mahakama itamtia hatiani mtuhumiwa", amesema Hakimu Mbuya




Katika utetezi wake Boi alidai, Februari 8,2019 alikuwa nyumbani kwake amelala ndipo aliamshwa na muito wa simu aliyopigiwa na mwanae aliyemtaja kwa jina moja la Kulwa ambaye baada ya kupokea kupokea alimwambia kuwa Abas Mwinjuma amefariki na yeye ndiye anayetuhumiwa kumuuwa.

Boi alidai kuwa mwanae Kulwa alimuita nyumbani kwake na akaamua kubaki kwa mtoto wake kwa ajili ya usalama wake.

Hakimu Mbuya akimuachia huru Boi amesema, sheria inavyo viwango vyake vya kupitisha makosa ya jinai lakini upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Boi Rajabu ndiye anayehusika na kifo Cha Rajabu mwinyijuma.

Katika kesi hiyo inadaiwa, Februari 8 2019, huko Mbweni mshtakiwa Bio alimuua jirani yake Abasi Mwinyijuma kwa kumchoma na kisu kutokana na ugomvi wa mipaka mahala wanaoishi.

Mwinyijuma alifariki usiku wa Februari 8,2019 akiwa njiani kupelekwa hospitali kwa matibabu.

Mtuhumiwa Boi Rajabu (60) katikati akiteta jambo na mawakili wake kabla ya kusomwa hukumu dhidi yake ya kesi ya kumuua Jirani yake Abasi Mwinyijuma kwa kutumia kisu. Hata hivyo Boi ameachiwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...