Na Petty Kidubo, Singida
Kata ya Mughanga katika Manispaa ya Singida imefanikisha programu ya utoaji chakula, kwa shule za msingi na sekondari zilizopo katika kata hiyo.
Mtendaji wa Kata ya Mughanga Bi. Futari Shauri amesema kuwa, kupitia ofisi ya Kata hiyo, tayari vikao vya kuwaelimisha wazazi na walezi, vimefanyika kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.
Mtendaji huyo amesema kuwa, wazazi na walezi kwa kauli moja wamekubaliana kuchangia kila mmoja Tshs. 10,000 kwa mwezi ili kuwezesha huduma ya chakula.
Shauri amefafanua kuwa, ulaji wa chakula kwa wanafunzi, utatolewa mara nne kwa wiki, na kuongeza kuwa mchango wa chakula kwa wazazi, utahusisha pia shule husika ambayo nayo italazimika kuchangia sehemu ya programu hiyo.
Amesema Kata ya Mughanga yenye shule mbili za Msingi na moja ya Sekondari, watoto watapatiwa chakula (makande), kwa wanafunzi wote wa Sekondari, na kwa shule za msingi mpango huo utahusisha darasa la pili mpaka la saba la saba.
Aidha, Shauri alibainisha kuwa, kwa wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza, wao watalazimika kunywa uji pekee, kutokana na muda wao wa masomo kukoma kila siku saa tano asubuhi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...