Mlezi wa Matembezi ya UVCCM ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mke wa Rais Zanzibar, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Rehema Omary Sombi na ujumbe wake waliofika Ofisi za ZMBF, Ikulu Migombani.
Mama Mariam Mwinyi amewataka UVCCM kuwa Mabalozi wa kitaifa kukemea vitendo vya udhalilishaji kwa Watoto na kuibeba kama ajenda ya Kitaifa wanapozunguka Mikoa ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.
Pia, Mama Mwinyi amewataka kuwa ubunifu zaidi Katika shamrashamra za matembezi ya kuadhimisha Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwakani kwa kuja na mbinu tofauti kwa kuibua miradi ya vijana kwa maendeleo na kuendelea kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .
Naye, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Sombi amempongeza Mama Mariam Mwinyi kwa kutimiza Mwaka mmoja wa Taasisi yake ya ZMBF, pia kwa mafanikio ya kazi nzuri kwa kuwawezesha wanawake, wakulima wa mwani, kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto na kuwa kinara wa hamasa katika kushiriki kuhamasisha ufanyaji wa Mazoezi katika matembezi ya Kila mwisho wa Mwezi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...