Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) - Taaluma, Prof. Boneventure Rutinwa (wa kwanza kulia) akiwa na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la JICA nchini Tanzania, Yamamura Naofumi (katika) na Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael wakionyesha baadhi ya nyaraka ambazo zinashinikisha masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Tanzania na Japan.
Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akitoa hotuba yake katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa akitoa hotuba yake katika Kongamano hilo


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) - Taaluma, Prof. Boneventure Rutinwa amesema kipindi cha nyuma Chuo hicho hakikuwekeza vya kutosha kwenye masuala ya ubunifu na uvumbuzi ili kusaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo sanjari na kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania, Prof. Rutinwa amesema kwa sasa wanashirikiana na Sekta husika za masuala hayo ya ubunifu na uvumbuzi ili kuhakikisha changamoto mbalimbali katika jamii zinatatuliwa na nchi kwa ujumla inapiga hatua kimaendeleo.

Prof. Rutinwa amesema mashirikiano yaliyopo sasa kati ya Tanzania na Japan, kongamano hilo linajadili uanzishwaji wa ‘programu’ ya mafunzo ambayo yataiwezesha Tanzania kupitia UDSM kujifunza kutoka kwa Japan na kupata uzoefu wao kama taifa lililoendelea bila kuiga na kufuata mbinu za Mataifa ya Magharibi.

Prof. Rutinwa amesema: “Ushirikiano huu wa nchi yetu Tanzania (UDSM) na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) sio kwenye teknolojia ya viwanda pekee, hata kwenye Sayansi ya Jamii katika lengo la kutatua matatizo na changamoto kwa jamii ya Watanzania na nchi kupiga hatua kimaendeleo.”

Prof. Rutinwa amesema kuwa awali kulikosekana mashirikiano mazuri baina ya Sekta husika (Industry Academia Linkages) ambazo tayari zimeendelea ili Tanzania kupitia Chuo hicho kujifunza na kusaidiana katika kubadilisha uzoefu wa masuala hayo ya maendeleo.

Awali, Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael alisema midahalo kwenye Kongamano hilo yaliangazia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutokana na mabadiliko yake, Serikali ya Tanzania imeweka nguvu zaidi katika masuala hayo kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu.

“Serikali inazingatia sana masuala ya TEHAMA katika kujenga ubunifu wa Watanzania, ndio maana Serikali tumeona kuna umuhimu kuanza kufundishwa kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu, hivyo hivyo lazima kuwa na muendelezo kulingana na matekwa ya dunia,” amesema Dkt. Francis

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...