
Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa (BASATA) Abel Ndaga akimkabidhi tuzo muasisi wa Tamasha la " Lady ina Red " Asia Khamsin kwa kutambulika mchango wake mkubwa kwenye sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Hugo Domingo Mario Frenandes akizungumza na Wanahabari wakati wa Kumalizika kwa Miaka 20 ya Jukwaa la Lady in Red Lililofanyika katika Ukumbi wa Warehouse Masaki Jiji Dar es Salaam, Hugo Domingo kama waandaji kwa misimu miwili mfululizo wa Tamasha hilo.
*Hugo Domingo wampa Tuzo Mama Asia
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
TAMASHA la ''Lady in Red'' lafanyika dar wabunifu na wanamitindo chipukizi wapatiwa tuzo kama pongezi ya Sekta ya ubunifu na wanamitindo kutambua mchango wao.
Akizungumza na Michuzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Hugo Domingo, Mario Frenandes ambao ndio waandaji wa onyesho hilo kwa Msimu wa pili amesema tamasha la "Lady in Red limekuwa moja ya jukwaa linalotoa fursa mbalimbali sekta ya ubunifu,wanamitindo, mapambano na Muziki.
"Huu ni msimu wa pili tunaendelea kuunga mkono jukwaa hili lengo ni kuwapa nafasi wenye vipaji kuonekana katika sekta mbalimbali na ndio hasa lengo la Hugo Domingo kuona vijana wanafanya kazi kutokana na ujuzi wao na hata kwenye Tamasha hili hatukubagua tumeshirikiana nao wanamuziki,washereheshaji na wasanii.
Fernandes amesema Tamasha hilo kwa mwakani wanatarajia kufalifanya kwa ukubwa sana na kushirikisha wabunifu kutoka nje huku Tamasha likitarajiwa kufanyika Visiwani zanzibar.
Ameeleza namna jukwaa hilo kwa mwaka huu kutimiza kwake miaka 20 tangu kuasisiwa na Mbunifu Mkongwe Mama Asia Khamsin imepelekea wao kama waandaaji wa jukwaa hilo kwa utofauti na kwa ukubwa zaidi.
"Mitindo sasa hivi inafanya vizuri mwakani tuna mpango wa kuanza visiwani Zanzibar na kilele chake kumalizika Dar es Salaam, hivyo wabunifu wajiandae kuonyesha mavazi yenye viwango vya juu zaidi."
Pia ameongeza kuwa wadau mbalimbali wa sekta ya Mitindo wa endelee kuunga mkono Tamasha hilo ili liendelee kuwepo kila mwaka kwa lengo la kuwaunga mkono wabunifu chipukizi pamoja na wanamitindo.
Katika Tamasha hilo liliweza kutoa tuzo ya Heshima kwa Muasisi wa tamasha hilo Mama Asia Khamsin kwa kutoa vipaji vingi ambavyo kwa sasa ni wabunifu wakubwa Afrika akiwemo Ally Remtullah,Noel stylish pamoja na wengine mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...