MOJA ya Mashirika makubwa ya uzazi wa mpango yalifanya tukio la kukutanisha wadau wa sekta hio mapema wiki hii kwenye ofisi za shirika Masaki, Dar es salaam.

Tukio ambalo lilikuwa na nia ya kubadilishana mawazo juu ya namna ya kukabiliana na mahitaji ya uzazi wa mpango nchini, lilihudhuriwa na Mashirika kama Engender Health, UMATI, Medicins Du Monde pamoja na wadau mbalimbali akiwamo Miss Tanzania Halima Kopwe.

Akizungumza kwenye hafla hio Mkuu wa Masoko wa DKT Tanzania Deogratius Kithama amesema “Shirika letu limejikita katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za uzazi wa mpango wa Mpango kama Kiss condoms na vidonge vya majira vya Trust Daisy ambavyo vinapatikana kwa bei nafuu sana”

Wakati kwa upande wake Miss Tanzania 2022 Halima Kopwe akiongelea umuhimu wa kuongeza elimu juu ya afya hususan kwa vijana ili waweze kufanya maamuzi sahihi juu ya miili yao .

Serikali ya awamu sita imeongelea juu ya umuhimu wa uzazi wa mpango , haswa baada ya Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kuelezea umuhimu wa “kupunguza spidi kwenye uzazi”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...