Na Khadija Seif, Michuzi TV
MWANGA Hakika Benki wazindua rasmi Kampeni ya "Mseleleko" kwa Wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali nchini wameombwa kujitokeza kwa wingi kuweka akiba katika benki ya Mwanga Hakika ili waweze kupata asilimia 12 ya faida kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.
Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 15,2023 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa katika benki hiyo ya Mwanga Hakika, Projest Massawe amesema Kampeni hiyo "Mseleleko " itadumu kwa muda wa Miezi mitatu kwa lengo la kuwapa faida wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara kupitia benki hiyo pale wanapoweka pesa zao .
Massawe amesema ili kuhakikisha wanawafikia wateja wengi zaidi benki imeamua kima cha chini cha uwekezaji ni kuanzia Shilingi 500,000 na kuendelea na kwamba kila kiwango atakachoweka mteja kitampatia fursa ya kupata faida mpaka asilimia 12 kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.
"Mteja atakayeweka amana katika benki yetu kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 atapata faida mpaka asilimia 12 kwa mwaka, tumekuja na kampeni hii ya Mseleleko Akaunti ambayo itakuwa ya miezi mitatu tunategemea tutawagusa watanzania wengi kwenye hii fursa ya kuweka akiba katika benki yetu na kupata gawio au faida mpaka asilimia 12 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Aidha Masawe ameeleza zaidi kuwa benki hiyo ambayo kwa sasa ina matawi saba nchi nzima itaweza kuwahudumia watanzania wote hata wale ambao bado matawi hayajafika kwa kutumia mtandao na simu banki.
"Mkakati wetu ni kuwekeza kwa wafanyabiashara na ndio maana tupo hapa kulihamasisha kundi hilo kuja na kupata faida ikiwemo ya kupata mkopo hadi asilimia 80 ya fedha ambayo amewekeza hapa kwetu."
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Biashara Wateja wa kati na wadogo katika benki hiyo, Joseph Samson amefafanua zaidi kwa mfanyabiashara au mjasiriamali atakayeweka akiba katika benki yao, moja ya kigezo anachotakiwa kuwa nacho ni awe mtu anayefanya shughuli inayokubalika na serikali.
"Pia atatakiwa kuweka kiasi hicho cha Sh. 500,000, fedha zake ziwekwe kwa muda usiopungua miezi sita pamoja na awe anafungu akaunti hii ya Mseleleko, anayehitaji huduma hii tutamfua hata nyumbani kwake kumuhudumia,".
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Wateja wa kati na wadogo katika benki hiyo, Joseph Samson (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vigezo ambavyo anatakiwa kuwa navyo atakaefaidika na Kampeni ya "Mseleleko " kutoka Benki ya Mwanga Hakika ya kupata gawio la Asilimia 12 leo Februari 15, 2023 katika Ofisi za Benki ya Mwanga Hakika Jijini Dar es salaam akifafanua
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa katika benki hiyo ya Mwanga Hakika, Projest Massawe (katikati) akizungumza na waandisi wa habari leo Februari 15,2023 mara baada ya kuzindua rasmi Kampeni ya "Mseleleko '' kwa wateja wapya pamoja na wa zamani wa Benki ya Mwanga Hakika ambapo watafaidika na gawio la Asilimia 12 kwa kima cha chini cha shilingi 500,000 ambapo Kampeni hiyo inalenga kuwagusa wajasiriamali na wafanyabiashara kuwekeza na kuhifadhi pesa zao katika benki hiyo yenye Matawi 07 nchi nzima
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...