NABU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kutumia ubunifu na weledi wake kusanifu mifumo itakayorahisisha utoaji huduma kwa wananchi ili kukabiliana na changamoto za kijiografia.
Ndejembi ametoa maelekezo hayo mkoani Iringa wakati alipotembelea Ofisi za eGA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kukagua utendaji kazi wake na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa ofisi hiyo.
Akizungumzia maeneo ambayo jiografia yake haipo vizuri, Ndejembi amesema maeneo hayo yanapaswa kuwa na miundombinu ya TEHAMA itakayowezesha upatikanaji wa huduma za kimtandao zilizosanifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.
Ndejembi ametoa maelekezo pia kwa Taasisi za Umma nchini kushirikiana na eGA katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma ili iweze kukidhi nahitaji na viwango katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
" Taasisi za umma itumieni Mamlaka ya Serikali Mtandao ipasavyo katika kutengeneza mifumo itakayokidhi viwango vya kutoa huduma bora kwa wananchi kwa lengo la kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwa na Serikali Mtandao," Amesema Ndejembi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...