Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
SIMBA SC imethibitisha kumkosa Mshambuliaji wao raia wa Ghana, Augustine Okrah baada ya kuumia katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Al Hilal SC ya Sudan, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin, jijini Dar es Salaam na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imeeleza kuwa Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema kuwa Mshambuliaji Okrah atachukua muda kuanza mazoezi na wenzake kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Horoya AC kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL), hatua ya makundi.

Hata hivyo, Simba SC imethibitisha kuwa Wachezaji wake, Jean Baleke na Pape Ousmane Sakho wanaendelea vizuri na wapo tayari kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Horoya AC. Baleke na Sakho walipata majeruhi kwenye mchezo huo dhidi ya Al Hilal kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo huo wa mzunguko wa Kundi C la Michuano hiyo utachezwa Februari 11, 2023 mjini Conakry nchini Guinea kwenye dimba la General Lansana Conté.

Baada ya kumaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal SC, Wachezaji wa Simba SC walipewa mapumziko ya siku moja na watarudi kambini Februari 7, 2023 kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea mjini Conakry nchini Guinea kwa ajili ya kipute hicho dhidi ya wenyeji Horoya AC kwenye Michuano hiyo ya CAF CL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...