MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za uwepo wa kimbunga “Freddy” zinazosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua taharuki kwa jamii.

Katika Taarifa yake iliyotolewa leo Februari 20, 2022 imesema, kwa takribani wiki sasa Mamlaka imekuwa ikifuatilia mwenendo wa kimbunga hicho, “Freddy” kilichopo kusini magharibi mwa bahari ya Hindi karibu na pwani ya Madagascar na kujiridhisha kuwa hakuna na madhara ya moja kwa moja kwa sasa kwa maeneo yaliyoko nchini kwetu.

Aidha taarifa hiyo imesema, kupitia sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania namba mbili ya mwaka 2019, Mamlaka imepewa jukumu kisheria kufuatilia na kutoa tahadhali za hali mbaya ya hewa kwa jamii. Taarifa hizi za hali mbaya ya hewa hutolewa kwa jamii pale tu zinapokuwa zimekidhi viwango na miongozo ya utendaji kazi.

Taarifa hiyo imesema, TMA, inaendelea kufuatilia kwa kina mwenendo wa kimbunga hicho na itatoa taarifa punde tu kutakapokuwa na haja ya kufanya hivyo.

Pia, Mamlaka inaikumbusha jamii na umma kwa ujumla kuwa kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya 2019, ni TMA pekee nchini ndiyo yenye mamlaka ya kutoa taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa na ni kosa kisheria mtu mwingine kufanya hivyo.

Hivyo wamewashauriwa wananchi kuendelea kuzingatia taarifa na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania sambamba na kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...