Na Khadija Seif, Michuzi Blog 
MSIMU wa 4 wa Shindano la "Hello Mr.Right" wafunguliwa rasmi huku washiriki wakifurika kwenye usahili wa Shindano hilo .

Akizungumza mapema Mkurugenzi wa Tv3 Ramadhan Msemo amesema Shindano hilo kwa Msimu huo wa 4 litakuwa lakitofauti kutoka na ingizo jipya la watangazaji pamoja na majaji.

'' Awali Mtangazaji wakike alikuwa Neema Aloyce kijiti chake kimechukuliwa na Ammygal huku kwa upande wa majaji wa usahili wakiwa wengi akiwema Mwijaku,Fatna ramole na wengine wengi.

Pia amesema kipindi hiko kitakuwa kikirushwa mubashara kupitia Startimes chaneli ya stbongo kila siku ya Jumamosi saa 4 usiku na marudia Jumapili.
Hata hivyo Mtangazaji wa Kipindi hicho Mc garaB amesema kumekuwa na Misemo mbalimbali tangu kuanza kwa Shindano hilo huku akiutaja misemo mbalimbali na kwa mwaka huu utatumika "Ni zamu yako''.

Kwa upande wa Mtangazaji Muendeshaji wa kipindi hiko ambae ni ingizo jipya ''Ammygal'' amesema kutokana na uwezo wake na kipaji alichonacho ndio sababu kubwa iliyowafanya waandaaji wa kipindi hiko cha vijana kuona anaweza kufaa na kuhaidi kuitumia jukwaa hilo kuongea na vijana wenzake katika Mahusiano na kutafuta mwenza sahihi kwa vigezo ambavyo watavihitaji.

"Nawapongeza Familia ya Startimes kupitia St bongo kwa kuniteua kuungana na Familia kubwa ili kufanikisha Shindalo hilo la "Hello Mr.Right. "

Pia kwa upande wake Mwijaku amesema anatarajia kipindi hicho kiwe ni sehemu ya kushuhudia ndoa nyingi pamoja na watoto ambao watatokana na Shindano hilo.

Nikiwa kama mzoefu katika ndoa yangu miaka 10 hili litakuwa jukwaa kubwa litakalonikutanisha na vijana wengi tuzungumze kuhusu Mahusiano pamoja na ndoa kwa ujumla.

Hata hivyo ametoa wito kwa wasanii mbalimbali kujitokeza katika jukwaa hilo kwa lengo la kutafuta wenza wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...