NA Yeremias Ngerangera….Namtumbo
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Ng’waniduhu Malenya aliwatoa hofu wananchi wa kijiji cha Masuguru walioonesha wasiwasi wao kuhusu kuliwa kwa fedha zilizotolewa na serikali kwa lengo la kujenga mradi wa maji katika kijiji cha Masuguru.
Malenya aliwatoa hufu wananchi hao kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika kijijini hapo, baada ya wananchi kuonesha wasiwasi wa kuliwa kwa fedha za ujenzi wa mradi wa maji kwa madai kuwa kiasi kilichotolewa na serikali shilingi milioni 510 ni fedha nyingi sana ukilinganisha mradi wenyewe.
Aidha mkuu wa wilaya huyo kabla ya kufanya mkutano , aliutembelea mradi huo na kujionea kazi zilizofanyika katika ujenzi wa mradi huo na kujiridhisha na kazi zilizofanyika katika kuutekeleza mradi huo wa maji.
Hata Hivyo Mkuu wa wilaya huyo aliwaambia wananchi hao kuwa ujenzi wa mradi huo utakuwa miongoni mwa miradi itakayopitiwa na mwenge wa uhuru 2023wilayani Namtumbo kwa lengo la kuuzindua mradi huo.
David Mkondya ni meneja kutoka wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini alitaja kazi zilizofanyika katika ujenzi wa mradi huo na kuwaambia wananchi hao kuwa miradi ya maji inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa inteki , matenki,ununuzi wa mabomba yanayotumika kulazwa kutoka chanzo mpaka kwenye matenki na ulazaji wa bomba kutoka kwenye matenki mpaka kijijini kwenye jamii ambako hujengwa vituo vya kupata huduma ya maji.
Mkondya alidai katika kijiji cha Masuguru kuna jumla ya vitongoji 6 na kati ya vitongoji hivyo ni kitongoji kimoja cha Namanima ambacho hakijapata huduma ya maji kutokana na kitongoji hicho kuwa mbali zaidi ya kilomita mbili ambako nako unavuka mto na makazi ya watu yapo kwenye mwinuko .
Hata hivyo Mkondya alifafanua kuwa kitongoji hicho kimeombewa fedha ili kichimbwe kisima kikubwa kitakacho tumika kujaza maji kwenye tenki na kisha kuwajengea vituo wananchi kwa ajili ya kupata huduma ya maji alisema Mkondya.
Ziara ya mkuu wa wilaya katika kijiji cha Masuguru wilayani Namtumbo ilikuwa ni kujitambulisha kwa wananchi,kusikiliza kero na kuzitolea ufafanuzi kero za wananchi baada ya kuteuliwa tena na mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa wilaya na kuhamishwa kutoka Wilaya ya Ulanga mkoa wa Morogoro na kuja Namtumbo mkoa wa Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...