Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeanza ziara yake tangu tarehe 15 Machi, 2023 katika Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga na kukagua Miradi miwili ya Maji inayosimamiwa na Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) na Mamlaka ya Maji ya Shinyanga (SHUWASA).
Miradi hiyo iliyokaguliwa yote inapokea maji kutoka mradi mkubwa unaotoka Ziwa Victoria unaosimamiwa na KASHWASA.
Miradi hiyo miwili ni mradi wa Kagongwa - Isaka kwenda vijiji vya Kilimbu, Jana, Butondolo na Itogwanholo.Mradi mwingine ni mradi wa maji katika Mji wa Tinde na Shelui.
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mheshimiwa Jackson Kiswaga (Mb) amesema Kamati imetidhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kuziagiza RUWASA na Mamlaka ya Maji (SHUWASA) kuangalia uwezekano wa kuongeza vituo vingine vya kuchotea maji ili wananchi wapate maji kwa ukaribu zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...