Kampuni 3 bunifuchipukizi kwenye masuala yakiteknolojia zimeibukawashindi wa programu ya msimu wa pili ya Vodacom Digital Accelerator. Washindi hawa walipatikana baada ya mchuano mkali na kuwasilisha shughuli za kampuni zao mbele ya majaji wabobevu na kupitia mchakato wa kupigiwa kura, ambapo watazawadiwa zaidi ya Shilingi milioni 200 za Kitanzania, zikiwa ni katika usimamizi wa miradi yao pamoja na kuongeza thamani na kutafutiwa uwekezaji Zaidi mbeleni.

Akizungumza wakati wa siku ya maonyesho ya kampuni hizo bunifu chipukizi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu ameipongeza Vodacom Tanzania PLC kwa jitihada za kuziibua kampuni chipukizi zenye mawazo bunifu ya kiteknolojia kutoa huduma na bidhaa ambazo zina fursa ya kuingia sokoni na kuwa na fursa ya kukua na kujiendesha kwa biashara.

“Ni jitihada za kupongezwa kwenye ukuzaji wa kampuni chipukizi za kiteknolojia nchini Tanzania, wote tunafahamu ambavyo maendeleo ya sayansi na teknolojia yalivyobadili hali ya Maisha ya watu kiuchumi na kijamii duniani kote. COSTECH tunazitambua jitihada hizi na milango yetu ipo wazi kwa ushirikiano zaidi.

 Ningependa kutoa wito kwa makampuni na wadau wengine nao aidha kujitokeza kuunga mkono jitihada hizi au kuanzisha program zenye malengo sawa na hii ili tuweze kuziibua kampuni chipukizi bunifu nyingi zaidi kwani bado changamoto nyingi za kijamii zinahitaji masuluhisho ya kiteknolojia ambapo kama nchi tunakuwa kwa kasi kwenye nyanja hii,” alisema Dkt. Nungu

Programu ya Vodacom Digital Accelerator inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc na kuendeshwa na kampuni ya SmartLab ni ya kipekee inayoendeshwa na kampuni binafsi katika sekta ya ubunifu Tanzania ambapo imeundwa maalum ili kukuza kampuni changa na kibunifu za kiteknolojia. 

Huu ni msimu wake wa pili ambapo maombi zaidi ya700 yamepokelewa tangu kuanzishwa kwake mwaka2019 huku kampuni 28 zikiwa sehemu ya programu hii na kupokea msaada katika kuwajengea uwezo wa mikakati yao ya kimasoko, eneo la kiufundi, na kuwaunganisha na wawekezaji na washirika. Kwa msimu huu wa pili, jumla ya kampuni 12 zilichaguliwa kutoka sekta tofauti kama vile huduma za teknolojia za kifedha, afya, biashara za mtandaoni, elimu, kilimo, na sekta ya usalama wa mtandaoni.

Mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa msimu wa pili wa programu ya Vodacom Digital Accelerator, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Phillip Besiimire alisema kuwa amefurahi kuona sekta ambazo zimeibuka washindi – kilimo, elimu, na usafirishaji zitapatiwa ufumbuzi kwani zinakumbwa na changamoto kadhaa ambazo teknolojia inaweza kutoa suluhisho.

“Nimefurahi kuona vijana wana mawazo yenye kuleta mapinduzi kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi, hii inaonyesha ari na mwelekeo wa taifa kwa ujumla. Lakini jambo la kipekee ambalo limenifurahisha ni kuona mwanamke ndiye ameibuka mshindi wa kwanza. Nadhani mmejionea wenyewe kuwa waanzilishi na washirika wa kampuni hizi chipukizi kwenye masuala ya teknolojia wengi wao ni wanaume. Hivyo, nitumie fursa hii kutoa wito kwa serikali na wadau kuangalia uwezekano kama tunaweza kuwa na programu ya aina hii mahususi kwa wanawake pekee.

 Hii itachochea kuwa na wanawake wengi waanzilishi lakini pia itaongeza fursa kwa wanawake nao kuwepo kwenye nafasi za juu kwenye mfumo wa uongozi kwenye kampuni hizi. Kwa kuongezea, kuwepo pia na majukwaa kama haya kwa ajili ya walemavu ili kuonyesha uwezo wao kwani bado wanasahaulika. Kuwepo kwa jukwaa lao maalum kutasaidia kuongeza ujumuishi kwenye ngazi zote za jamii,” alihitimisha Bw. Besiimire

“Ningependa kuzipongeza kampuni za BizyTech kupitia huduma yao ya Kilimo Bando, Smart Darasa, naTwenzao kwa kuibuka washindi na kampuni zote ambazo zimeshiriki msimu wa pili wa programu yaVodacom Digital Accelerator. Majaji walikuwa na wakati mgumu kuchagua mshindi kwasababu wote mlikuwa na mawazo bunifu na pekee ya kibiashara.

Inatia moyo kuona vijana wana suluhu za kiteknolojia ambazo zinaweza kujiendesha kwa faida. Ninatumaini kuwa mafanikio yatakayopatikana baada yahatua ya leo yatakuwa ni chachu kwa kampuni zingine chipukizi si tu kwa kuwapatia Watanzania suluhusho la changamoto mbalimbali zinazowakabili lakini pia itawashawishi kujitokeza zaidi kushiriki programu hii na kujifunza kutoka kwenu,” alisema Mkurugenzi waKidigitali na Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando.

Bw. Nguvu alizitaka kampuni zingine kuja na programukama hizi kwani zinahamasisha kampuni nyingi zaidikujitokeza ambapo hitaji bado ni kubwa.

“Tumepokea mamia ya maombi lakini hatukuweza kuyatosheleza yote. Hivyo tunaiomba serikali kulitazama jambo hili kwa ukaribu na kusaidia kutoa motisha kwa makampuniambayo yanasaidia jitihada kama hizi ili kuongeza hamasa na kushirikiana nasi katika kuzisaidia kampuni chipukizi nyingi zaidi za kiteknolojia,” alihitimisha.

Kwa upande wake Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bizy Tech ambao kupitia huduma yao ya Kilimo Bando imeibuka mshindi wa kwanza Isabella Fernandes amesema, “ulikuwa ni wakati wa kipekee kushiriki na kupata fursa ya kuwasilisha na kuonyesha shughuli ambazo kampuni yetu pamoja na washiriki wengine. Pamoja na kutangazwa kuwa mshindi, ninaamini kuwa sasa Tanzania imefikia hatua ambayo kampuni zake chipukizi za kiteknolojia zinaweza kuchuana kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa.

Kampuni hizi zilizowasilisha mawazo yao leo zinastahili fursa ya kuingia sokoni. Ni matumaini yangu tutapata fursa ya kukutanishwa na washirika na wadau walioandaliwa na waandaaji wa programu hii ili kuhakikisha ndoto zetu zinatimia,”

Programu ya Vodacom Digital Accelerator msimu wa pili chini ya Vodacom Tanzania PLC imefanyika kwa kushirikiana na SmartLab ambao watahusika na programu maalum ya kuzisimamia na kuzijengea uwezo kampuni zilizoibuka washindi kwa muda wa miezi sita.

Ndani ya muda huo washindi watapokea fedha ambazo hazitowalazimu kutoa umiliki kwa wawekezaji, ufuatiliaji wa uwekezaji, fursa ya kushirikiana na M-Pesa kwenye huduma zao, kuunganishwa na wataalamukwenye sekta husika, kuunganishwa na nyenzo za mafunzo, kusaidiwa kwenye masuala ya sera na udhibiti, msaada wa kiteknolojia, na namna ya kuingia sokoni.

Kampuni bunifu chipukizi ambazo zimefikia hatua yafainali ni pamoja na Shule Yetu Innovations, Smart Darasa, Lango Academy, na Vijana Tech, kwa upandewa huduma za elimu za kiteknolojia. Hack it Consultancy inawakilisha eneo la huduma za usalamawa mtandaoni. Seto, Twenzao, Get Value, na SpidiAfrica zipo chini ya biashara za mtandaoni. Nyinginezoni Medpack ikiwakilisha huduma za afya za kiteknolojia, zikiwemo na, Bizy Tech Pamoja na BizzyPay ambazo zenyewe zipo upande wa huduma za kifedha za kiteknolojia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire (kulia) akimkabidhi tunzo ya mshindi wa kwanza wa awamu ya pili ya programu ya Vodacom Digital Accelerator Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya BizyTech kupitia huduma ya Kilimo Bando, Bi. Isabella Fernandes (kushoto). Washindi watatu walipatakana kutoka miongoni mwa kampuni 12 zilizoshiriki ambapo watakabidhiwa zaidi ya milioni 200 za Kitanzania kuendesha kampuni zao. Wakishuhudia tukio hilo kulia na kushoto ni jopo la majaji ambao walishiriki kwenye mchakato wa uwasilishaji na kuchagua washindi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire (mwenye kipaza sauti) akizungumza na washiriki na wageni waalikwa (hawapo pichani) mara baada ya kutangazwa kwa washindi watatu wa awamu ya pili ya programu ya Vodacom Digital Accelerator ambapo kampuni tatu chipukizi bunifu za kiteknolojia – BizyTech kupitia huduma yao ya Kilimo Bando, Smart Darasa, na Twenzao ziliibuka washindi. Washindi watatu walipatakana kutoka miongoni mwa kampuni 12 zilizoshiriki ambapo watakabidhiwa zaidi ya milioni 200 za Kitanzania kuendesha kampuni zao, hafla ya uwasilishaji na utoaji tunzo hizo ilifanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.





Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire (wan ne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi pamoja na majaji wa awamu ya pili ya programu ya Vodacom Digital Accelerator ambapo kampuni tatu chipukizi bunifu za kiteknolojia – BizyTech kupitia huduma yao ya Kilimo Bando, Smart Darasa, na Twenzao ziliibuka washindi. Washindi watatu walipatakana kutoka miongoni mwa kampuni 12 zilizoshiriki ambapo watakabidhiwa zaidi ya milioni 200 za Kitanzania kuendesha kampuni zao, hafla ya uwasilishaji na utoaji tunzo hizo ilifanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...