Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV -Manyara
CHAMA Chama Mapinduzi (CCM) kimetoa maelekezo kwa Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Kilimo kukaa na kujadiliana namna uendeshaji wa mashamba ya ngano ya Basotu yaliyopo wilayani Hanang mkoani Manyara yatakavyotumika kuzalisha ,kwani kwa sasa hazalishi.
Kwa mujibu wa CCM ni kwamba mashamaba hayo yalikuwa yakisifika kwa kuzalisha zao la ngano kwa wiki lakini baada ya mashamba kuchukuliwa na Hazina yameacha kutumika kuzalisha ngano ,hivyo umefika wakati wa kuona yanazalisha.
Maelekezo hayo yametolewa na Chama hicho kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mashamba ya ngano Basotu.
"Mashamba haya sasa yawe chini ya Wizara ya Kilimo ili isimamie uzalishaji wa ngano kama ilivyokusudia na kuongeza upatikanaji wa bidhaa hiyo hapa nchini badala ya kuagiza nje ya nchi. Mkoa wa Manyara ulikuwa ukizalisha ngano kwa wingi hasa kule Basutu, lakini mashamba hayo yalichukuliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na tangu wakati huo hayazalishi tena.
"Hivyo natoa maelekezo kwa Serikali, Wizara ya Fedha na Wizara ya Kilimo, ndani ya wiki mbili wakubaliane na kukabidhiana mashamba yale ili yasimamiwe na Wizara ya Kilimo ambayo ndiyo imepewa jukumu la kusimamia sekta ya kilimo, haiwezekani tuwe na mashamba makubwa ya ngano lakini tunaagiza ngano nje ya nchi,"amesema Chongolo.
Amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mbulu na Mkoa wa Manyara kwa ujumla kwamba maelekezo na maagizo yake Kwa Serikali kupitia Wizara hizo mbili yatafanyiwa kazi haraka ili mashamba hayo uaanze kutumika kuzalisha ngano."Naamini mwaka huu ngano itaanza kuzalishwa."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...