Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfano wa barabara yenye alama muhimu za usalama barabarani katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Machi 14, 2023. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima na wa tano kulia ni Kamishina Jenerali wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Sixbert Reuben na kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Jamal Babu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Boniface Mkumbo (kushoto) ambaye alitoa maelezo kuhusu alama mbalimbali za barabarani zinazozingatiwa katika ujenzi wa barabara ili kuepusha ajali. Alikuwa kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Machi 14, 2023. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambako alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kwenye viwanja vya Furahisha, Machi 14, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkaguzi wa Polisi, Dumu Mwalugege (kulia) ambaye alitoa maelezo kuhusu alama za usalama barabarani katika maonyesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalam Barabarani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahish jijini Mwanza, Machi 14, 2023. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima na wa pili kushoto ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteremka kutoka kwenye basi baada ya kulikagua akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Machi 14, 2023. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...