Na.Khadija Sef,Michuzi TV
PAMBANO la marudiano la mabondia, Mfaume Mfaume kutoka Mabibo na Iddi Piarali wa Manzese linatarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Awali pambano hilo lilivunjika baada ya kupigana vichwa na Piarali kupata jeraha juu ya paji la uso na kusababisha kutoka kwa damu nyingi kitendo kilichosababisha pambano hilo kukatika.

Akizungumza na Michuzi Jijini Dar es Salaam katika zoezi la kusaini mkataba wa pambano hilo lililopewa jina la " King of the Night" Promota Khamisi Mrisho, amesema mabondia hao watagombani mkanda wa Ubingwa wa (WBF) uzito wa kati pambano la raundi 12.

Aidha Mrisho ameeleza kuwa lengo la kurudia pambano hilo ni kutafuta mbabe wa Dar es Salaam na bingwa wa WBF.

“Wadau na mashabiki wa mabondia wategemee kurudiwa kwa pambano hilo Septemba mwaka huu."

Bondia, Idd Piarali ameongeza kuwa anatarajia kuingia kambini hivi karibuni kujiandaa na pambano hilo.

“Watanzania wategemee burudani kutoka kwangu, dua zao muhimu ili niwe na nguvu na afya nzuri mimi na mpinzani wangu Mfaume Mfaume,” alisema Piarali.

Bondia Mfaume Mfaume amesema wadau na mashabiki zake wategemee ushindi wa mapema, kutokana na mazoezi anayoendelea kuyafanya.

Hata hivyo Pambano lao la awali Lililofanyika disemba 25,2022 Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) walivunja kutokana na mpinzani wake, Piarali kupata jeraha juu ya paji uso hivyo pambano la marudiano mashabiki wanahitaji matokeo ya kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...