Na.Khadija Seif, Michuzi Blog
FAINALI la shindano la kumtafuta mlimbwende wa Miss Tanga linatarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu Mkoani Tanga.

Akizungumza na Wanahabari Leo machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam jana Mratibu wa shindano hilo, Victoria Martin, ambaye pia ni mbunifu wa mavazi amesema usahili wa warembo utafanyika Machi 18,2023 katika Ukumbi wa Tanga Resort.

Aidha ameeleza kuwa shindano hilo litakuwa na utofauti na mashindano mengine ya miss ambayo yanafanyika hapa nchini kutokana na uzoefu aliokuwa nao katika upande wa tasnia ya urembo na mitindo.

“Nimeshatwaa taji la miss Tanga mwaka 2007 nafahamu sheria na kanuni za shindano la urembo, hivyo nitahakikisha warembo kutoka nyumbani Tanga wanatimiza ndoto zao kupitia ulimbwende."

Mratibu huyo ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa usahili kwa warembo wataingia kambini, Machi 29 mwaka huu kujifunza mambo mbalimbali ya urembo.

“Wito wetu kwa wadhamini kutusapoti ili kutimiza ndoto za wadogo zetu katika sekta ya urembo, pia kupeperusha vema bendera ya Taifa katika mashindano ya Kimataifa,”.

Martin amesema kipindi warembo watakuwa kambini watapata nafasi ya kutembea vivutio vilivyopo katika mkoa wa Tanga.
Mratibu wa Shindano la Miss Tanga Victoria Martin akizungumza na Wanahabari Leo Machi 16,2023 Jijini Dar es salaam wakati akitangaza rasmi ujio wa Shindano la Miss Tanga ambapo linatarajiwa kutamatishwa Mei 06,2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...