Na Jane Edward, Arusha

Jitihada za serikali na wadau katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungu zimeendelea kuzaa matunda,ambapo kwa Mkoa wa Arusha idadi ya vifo imefikia vifo Sitini na moja kati ya wakinamama sitini na tisa elfu mia moja na tisini na tisa waliojifungua kwa mwaka 2022.

Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi wa huduma ya M-Mama katika hospital ya Rufaa ya Mkoa ya Mt Meru Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Vones Uiso amesema zoezi hilo limekuja wakati muafaka.

Amesema vifo vya mama na mtoto ni moja wapo ya jambo lililokuwa linawanyima usingizi lakini kutokana na jitihada za serikali wameweza kupunguza kwa kiasi kikubwa.

"Ujio wa M-Mama sisi kwetu tunaona kama Mkombozi katika masuala ya uzazi na hii itarahisisha huduma za kina mama kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano"Alisema

Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, afisa Elimu Mkoa wa Arusha Abel Tupwa anasema wahudumu wa afya watakaotumia Mfumo huo,kuwajibika kikamilifu na kufuata maadili ya taaluma yao katika kutoa huduma.

Amebainisha kuwa wapo baadhi ya watumishi wanakosa weledi wakati wa utoaji wa huduma lakini kwa program hiyo ni vema kama wakiwa na nidhamu ya kazi .

Amewashukuru Vodacom kwa kujitoa kushiriki katika huduma hiyo muhimu na kwamba wadau mbalimbali wajitokeze ili kuweza kufikisha mbali huduma hiyo ambayo inasaidia maelfu ya watanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Vodacom pamoja na Pathfinder George Venant Anatoa hamasa kwa jamii kutumia fursa ya huduma ya M-Mama ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Anasema wao kama Vodacom wanajisikia furaha kuwa Miongoni kwa watu wanao okoa maisha ya mama na mtoto kwa kutumia teknolojia ya simu kiganjani.

Aidha amesema kama wadau lengo lao ni kuhakikisha huduma hii inazidi kwenda mbele na kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kutokomeza vifo vya mama na mtoto kwa kutumia ubunifu huu

Mratibu wampango wa Usafirishaji wa dharura kwa mama na mtoto mchanga mkoa wa Arusha Getrude Underson anasema huduma hiyo imekuwa ya kisasa kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Anasema kuwa mpango huo utasaidia kutumia madereva Jamii katika Mkoa wa Arusha ili kuweza kurahisisha huduma hiyo kwa haraka.

Uzinduzi wa huduma ya M-mama kwa Mkoa wa Arusha unafanya kuwa Mkoa wa tisa kufikiwa na huduma hiyo.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha afisa elimu Mkoa wa Arusha akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa program ya M-Mama.


Wakielekea kituo cha huduma ya M-Mama.

Picha ya pamoja wadau wa M-Mama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...