Na Mwandishi wetu Mirerani

MBUNGE wa Simanjiro Mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka amemtaka Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya kaskazini Godbless Lema kutokuahadaa wafanyabiasha wa madini ya Tanzanite wa jijini Arusha kutwa soko la Tanzanite litaruodhawa Arusha kutoka Mirerani kwani ni sawa na kudandia treni kwa mbele.

Ole Sendeka akizungumza kwenye ziara ya Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo mji mdogo wa Mirerani amesema biashara ya madini ya Tanzanite haitahama Mirerani kamwe.

"Lema asidandie treni kwa mbele kwa kuwaongopea wana Arusha kuwa soko la madini ya Tanzanite litahama Mirerani lirudi Arusha hilo halitafanyika," amesema Ole Sendeka.

"Kazi halali huwezi kuita ni laana kwani shughuli zozote za halali zinazomsababisha mtu kipato na kufanya mkono wa mtu uende kinywani huwezi kusema ni laana," amesema Ole Sendeka na kuongeza;

"Yeye amewadharau bodaboda mara viongozi wa dini, sasa anatapatapa kwenye Tanzanite, ametoka huko Canada tunatambua anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo,"

Hata hivyo, Chongolo akikagua jengo la Tanzanite City Mirerani amesema wananchi wa mji mdogo wa Mirerani wasihofie maneno ya uzushi juu ya soko la madini ya Tanzanite.

"Hata hivyo CCM siyo chama cha kujibizana na wanasiasa ila wanaoota mchana waacheni waote kwani serikali ya CCM haiwezi kujenga jengo kubwa la soko la madini Mirerani kisha lihamishe.

"Mirerani hivi sasa mpo kwenye jiji la Tanzanite na jengo lilikamilika mtafurahia matunda ya rasilimali hii ambayo duniani inapatikana eneo hili pekee," amesema Chongolo.

Machi 4 mwaka 2023 Lema akiwa jijini Arusha alizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa soko la Tanzanite halipaswi kuwa Mirerani pekee.

Julai 7 mwaka 2021 Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akizungumza mji mdogo wa Mirerani aliagiza biashara ya Tanzanite ifamyike Mirerani pekee ili kuuinua kiuchumi mji huo na kudhibiti utoroshaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...